Kazi ya uboreshaji wa miundombinu ya maji imetekelezwa na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) eneo la Msolwa kata ya Bwilingu Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze.
Kazi hiyo imehusisha matengenezo katika bomba la inchi 6 lililopata hitilafu.Kukamilika kwa matengenezo hayo kumerejesha huduma katika maeneo ya Msolwa, Mdaula, Chang'ombe na Matuli.