Breaking

Wednesday, 29 May 2024

DAWASA MTAANI KUFUATILIAJI MAKUSANYO YA ANKARA ZA MAJI



Zoezi la ufuatiliaji wa malipo ya huduma za maji kwa wateja wa madeni ya muda mrefu na muda mfupi ikiendelea katika mkoa wa kihuduma DAWASA Kinondoni.

Zoezi hili linaenda sambamba na utoaji wa elimu ya matumizi sahihi ya maji, utunzaji wa vyanzo vya maji, ulinzi wa miundombinu ya maji, umuhimu wa kulipa bili za maji kwa wakati pamoja na kusitisha huduma kwa wateja wenye malimbikizo ya madeni ya bili.

Mamlaka inasisitiza wananchi kulipa bili zao kwa wakati ili kuepukana na usumbufu wa kusitishiwa huduma kutokana na bili kutolipa kwa wakati.







Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages