Kazi ya kubadilisha miundombinu ya Majisafi ikitekelezwa na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) katika eneo la Bunju A , kata ya Bunju Wilaya ya Kinondoni.
Kazi hii itasaidia kuboresha huduma kwa wateja zaidi ya 100 kwa kuwapatia huduma bora na yakutosheleza ya Majisafi pamoja na kumaliza changamoto ya maji uliosababishwa na uchakavu wa miundombinu hiyo.