Breaking

Wednesday, 29 May 2024

BASHUNGWA AWEKA WAZI MIRADI ITAKAYOONDOA MSONGAMANO WA MAGARI KATIKA MAJIJI.

Serikali itaendelea na utekelezaji wa miradi inayolenga kuondoa kero ya msongamano wa magari katika majiji.

Haya yamebainishwa na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa wakati wa kuwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2023/25 Bungeni Dodoma.

Amesema miradi hiyo ni pamoja na mradi wa upanuzi wa barabara ya Mwanza-Usagara-Daraja la JPM kuwa njia 4 (km 37): Sehemu ya Mwanza – Usagara (km 22).

Pia, mradi wa mabasi yaendayo haraka (BRT) awamu ya tatu ambao unahusisha barabara ya Nyerere kuanzia makutano ya barabara ya Kivukoni na Mtaa wa Azikiwe hadi Gongolamboto (km 23.33).

Bashungwa amesema pia mradi wa BRT awamu ya 4 (km 30.12) utakaohusisha barabara ya Ali Hassan Mwinyi-Morocco-Mwenge -Tegeta; na kipande cha Mwenge-Ubungo.

Amesema pia ujenzi wa BRT Awamu ya 5 (km 27.6) ambao unahusisha barabara ya Mandela kuanzia makutano ya Ubungo-Bandari, makutano ya Mandela/Tabata-Tabata Segerea na Tabata-Kigogo.

Pia upanuzi wa barabara ya Mbagala Rangitatu-Kongowe (km 3.8) na daraja la Mzinga na upanuzi wa barabara ya Mwai – Kibaki (km 11.6).

Amesema pia upanuzi wa barabara ya Uyole-Ifisi-Songwe Airport jijini Mbeya yenye urefu wa kilometa 36 kutoka njia 2 kuwa njia 4.

Pia ukamilishaji wa ujenzi wa barabara ya mzunguko katika Jiji la Dodoma unaohusisha ujenzi kwa kiwango cha lami barabara ya mzunguko wa nje yenye jumla ya urefu wa kilometa 112.92 na ujenzi wa barabara hapa Dodoma ya mzunguko wa ndani (km 6.3).

Bashungwa amesema pia ujenzi wa barabara ya mzunguko wa kati Dodoma (km 47.2), upanuzi wa barabara ya Dodoma0Morogoro eneo la Bunge hadi Mji wa Serikali Mtumba.

Pia ujenzi wa barabara za mchepuo za Singida (km 46), Iringa (km 7), Kilimanjaro na Songea (km14.4).
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages