Breaking

Monday, 27 May 2024

BASHUNGWA AKAGUA MAONESHO YA SEKTA YA UJENZI - BUNGENI

Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa, amekagua mabanda ya Maonesho ya Sekta ya Ujenzi ambayo yanalenga kutoa elimu na huduma kuhusu kazi zinazofanywa na Wizara ya Ujenzi na Taasisi zake.

Maonesho hayo yanayotanyika kwa siku mbili katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma kuanzia leo Mei 27, 2024 hadi Mei, 28 mwaka huu.

Maonesho hayo yataambatana na uwasilishwaji ya makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka 2024/25 ambayo itasomwa Mei, 29 - 30, 2024 bungeni jijini Dodoma.

Katika maonesho hayo wabunge na wananchi watapata fursa ya kujifunza na kuzifahamu kwa ufasaha kazi zilizofanywa na tasisi zote zilizopo chini ya Wizara ya Ujenzi kwa kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages