Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) imekamilisha kazi ya maboresho ya miundombinu ya maji katika eneo la Mto Mzinga uliopo Mtaa wa Bombambili katika kata ya Majohe Wilaya ya Ilala.
Akizungumzia maboresho hayo, Mhandisi wa DAWASA Ukonga, Juma Kalemera amesema kuwa kazi hiyo imehusisha ubadilishaji na uhamishaji wa bomba la inchi 6 lililopo katika eneo la darajani kwa Fundi na kwa Butu.
"Maboresho yamelenga kuondoa bomba lililokuwa linapita chini ya Mto Mzinga na kulipitisha juu ya daraja kwa sababu mara nyingi bomba hilo likikuwa likisombwa na maji pindi mvua zikinyesha hivyo kusababisha adha ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa wakazi wa maeneo hayo." Ameeleza Mhandisi Kalemera.
Ameongeza kuwa kuwa DAWASA imeadhimia kubadili bomba ya zamani aina ya *UPVC* na kuanza kutumia bomba gumu na imara zaidi aina ya *HDPE* ili kuongeza uhakika wa upatikanaji wa huduma kwa wateja takriban wanaohudumiwa na bomba hilo."
Maboresho yatasaidia kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji katika Kata ya Majohe katika Mtaa wa Bombambili hususan maeneo ya *Kwa Fundi, Kwa Butu, Burawayo, Kavishe, Kwa Almaumdi, Mnase, Shuleni, Kwa Osama, Kwa masista, Gisela, Mbozi road na Kwa Sadam*
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990