Wanawake wa Wizara ya Nishati, wameungana na wanawake wenzao dunia kuadhimisha siku ya wanawake ambayo Mkoani Dodoma imeadhimishwa wilayani Chamwino.
Katika madhimisho hayo watumishi wametumia siku hiyo kuelimisha wananchi mbalimbali kuhusu nishati safi ya kupikia.
Akitoa elimu kwa baadhi ya wananchi Joyce Msangi afisa Misitu, alisema utumiaji wa nishati safi ya kupikia unalinda afya za walaji na inamuepusha mtumiaji na madhara mbalimbali
Aliyabainisha madhara hayo, ni pamoja na adhari kwenye mfumo wa upumuaji na inaharibu mazingira yanayotuzunguka.
Naye, Talkisia Erio Afisa Kumbukumbu, amewahimiza wanawake wa Dodoma kutumia nishati safi ya kupikia ili kuweza kujikwamua kiuchumi.
Kwasababu matumizi ya nishati safi ya kupikia yanauwezo wa kuhudumia watu wengine kwa muda mchache na kufanya mambo mengine ya kujikwamua kiuchumi.
Aidha, wanawake hao wamewashukuru watumishi hao na kuahidi kwenda kufanyia kazi elimu hiyo waliyoipata.
Katika Madhamisho hayo, yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya Chinagali Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990