Breaking

Wednesday, 13 March 2024

WANANCHI VISIWANI ZANZIBAR WAKABIDHIWA MITUNGI YA KUPIKIA 700 YA GESI YA ORXY

NA MWANDISHI WETU

KATIKA muendelezo wa utekelezaji wa mkakati wa matumizi ya nishati safi ya kupikia uliozinduliwa na Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango hivi karibuni, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, amekabidhi mitungi 700 ya gesi ya kupikia iliyotolewa na kampuni ya Oryx Gas Tanzania.

Akizungumza wakati wa hafla ya ugawaji wa mitungi hiyo iliyoambatana na semina juu ya matumizi sahihi ya gesi ya kupikia, aliwataka wananchi wa jimbo la Kikwajuni, Masauni aliwataka wananchi hao kuunga mkono mkakati huo kwani una faida kiafya, kiuchumi na kijamii.

Alieleza kuwa matumizi ya gesi mbali ya kuokoa muda katika mapishi, huondoa matumizi ya kuni na mkaa hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa athari za mabadiliko ya tabia nchi.

"Agenda ya nishati  safi ya kupikia ni muhimu kiuchumi wa familia kwani mbakibya kuepusha madhara ya kiafya kama ilivyoelezwa na wataalamu pia huokoa miti ambayo husaidia kupunguza joto ambalo ni miongoni mwa athari za mabadiliko wa tabia nchi", alieleza Mhandisi Masauni ambaye pia ni Mbunge wa jimbo hilo.

Aidha aliupongeza uongozi wa kampuni ya gesi ya Oryx kwa kuunga mkono mkakati huo na kuwapatia wananchi jimbo hilo ili kubadilisha maisha yao.

"Tunawapongeza kwa kutupatia watu wa Kikwajuni mitungi hii ambayo itawasaidia wananchi wetu kuimarisha maisha yao na ningeomba sisi tuliopatiwa mitungi hii tuwe mabalozi wa kuhamasisha matumizi ya gesi lakini pia kuitangaza kampuni hii kama njia ya kurudisha shukrani kwao", alieleza Masauni.

Awali akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania, Benoit Araman, alieleza kuwa kampuni yake imeibeba ajenda hiyo kwa kutekeleza miradi mikubwa nchini Tanzania hasa Zanzibar ili kuwanufaisha wananchi wa maeneo mbali mbali.

Akitaja faida za kutumia gesi ya kupikia ya Oryx, Araman alieleza kuwa ni pamoja na kuondoa hatari za kiafya kwa watumiaji wa wa kuni na mkaa kama nishati ya kupikia lakini pia hatari za kimazingira na ustawi wa jamii.

"Takribani watu 33,000 wanapoteza maisha nchini Tanzania kwa maradhi yanayotokana na kuvuta moshi unaotokana na mkaa au kuni hiyo ndio sababu ya Oryx gas kuja na suluhisho la kuwahamasisha wananchi kutumia gesi kwa matumizi ya kupikia", alieleza Araman.

Aliongeza kuwa matumizi ya gesi yanaepusha wamama na watoto kuumika kubeba kuni  hivyo kuepuka kujeuriwa na wanyama wakali wakiwa katika harakati za kutafuta kuni pia kuimarisha maisha ya wanawake na kuwalinda dhidi ya vitendo vya udhalilishaji.

“Kuanzia mwezi wa saba mwaka 2021 tumekuwa mstari wa mbele kuunga mkono utekelezaji wa mkakati wa serikali uliopewa nguvu na Raisi wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania , Dk. Samia Suluhu Hassan kwa lengo kwamba ifikapo mwaka 2033 asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia”, alieleza Araman.

Nae Katibu Tawala wa wilaya wa wilaya ya Mjini Unguja, Dk. Said Haji Mrisho, alieleza kuwa serikali inafanya jitihada mbali mbali kuwawezesha wananchi kutumia nishati mbadala ya kupikia hivyo aliwapongeza Oryx Gas kwa msaada wanaoutoa katika kubadili mitazamo ya jamii juu ya matumizi ya gesi safi ya kupikia.

Alieleza kuwa mipango ya kampuni hiyo kutokomeza matumizi ya nishati ya kuni na mkaa ambayo ina madhara ya afya inapaswa kuungwa mkono na kuwahimiza wananchi wa wilaya hiyo kupunguza matumizi ya kuni na mkaa.

Katika hafla hiyo Waziri Masauni mbali ya kukabidhi mitungi hiyo, pia aligawa sadaka kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani na vifaa vya michezo kwa ajili ya mashindano ya ‘Masauni Jazzira Cup’ inayofanyika katika mwezi wa Ramadhani.
Mama lishe wa visiwani Zanzibar wakiwa katika hafla ya ugawaji wa mitungi 700 ya kupikia ya Oryx kwa baba lishe na mama lishe Machi 13, 2024 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Visiwani Zanzibar.Mitungi hiyo imekabidhiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Yusuf Masauni kwa kushirikiana na Kampuni ya gesi ya Oryx.
Mama lishe wa visiwani Zanzibar wakiwa katika hafla ya ugawaji wa mitungi 700 ya kupikia ya Oryx kwa baba lishe na mama lishe Machi 13, 2024 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Visiwani Zanzibar.Mitungi hiyo imekabidhiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Yusuf Masauni kwa kushirikiana na Kampuni ya gesi ya Oryx.
Katibu Tawala Wilaya ya Mjini Dkt. Said Haji Mrisho akizungumza katika hafla ya ugawaji wa mitungi 700 ya kupikia ya Oryx kwa baba lishe na mama lishe Machi 13, 2024 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Visiwani Zanzibar.
Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Yusuf Masauni akizungumza katika hafla ya ugawaji wa mitungi 700 ya kupikia ya Oryx kwa baba lishe na mama lishe Machi 13, 2024 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Visiwani Zanzibar.
Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Benoit Araman akizungumza katika hafla ya ugawaji wa mitungi 700 ya kupikia ya Oryx kwa baba lishe na mama lishe Machi 13, 2024 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Visiwani Zanzibar.
Baadhi ya mitungi ya kupikia ya Oryx ambayo imekabidhiwa kwa baba lishe na mama lishe Machi 13, 2024 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Visiwani Zanzibar. Mitungi hiyo imekabidhiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Yusuf Masauni kwa kushirikiana na Kampuni ya gesi ya Oryx
Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Yusuf Masauni (wa pili kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Benoit Araman (wa kwanza kushoto) wakimkabidhi mtungi wa kupikia wa gesi ya Orxy Haroub Ali Abdallah katika hafla ya ugawaji wa mitungi 700 ya kupikia ya Oryx kwa baba lishe na mama lishe Machi 13, 2024 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Visiwani Zanzibar.
Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Yusuf Masauni (wa pili kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Benoit Araman (wa kwanza kushoto) wakimkabidhi mtungi wa kupikia wa gesi ya Orxy Rahima Bakari katika hafla ya ugawaji wa mitungi 700 ya kupikia ya Oryx kwa baba lishe na mama lishe Machi 13, 2024 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Visiwani Zanzibar.


Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Yusuf Masauni (wa pili kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Benoit Araman (wa kwanza kushoto) wakimkabidhi mtungi wa kupikia wa gesi ya Orxy Adhuruu Makame Kombo katika hafla ya ugawaji wa mitungi 700 ya kupikia ya Oryx kwa baba lishe na mama lishe Machi 13, 2024 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Visiwani Zanzibar.

Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Yusuf Masauni (wa pili kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Benoit Araman (wa kwanza kushoto) wakimkabidhi mtungi wa kupikia wa gesi ya Orxy Hudhaima Shaban Sururu katika hafla ya ugawaji wa mitungi 700 ya kupikia ya Oryx kwa baba lishe na mama lishe Machi 13, 2024 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Visiwani Zanzibar.

Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Yusuf Masauni akiwa pamoja na Katibu Tawala Wilaya ya Mjini Dkt. Said Haji Mrisho na Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Benoit Araman wakiwa kwenye picha ya pamoja na baba lishe na mama lishe wa visiwani zanzibar wakati wa hafla ya ugawaji wa mitungi 700 ya kupikia ya Oryx kwa baba lishe na mama lishe Machi 13, 2024 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Zanzibar.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Gesi ya Orxy, Peter Ndomba akitoa elimu ya matumizi ya mtungi wa kupikia wa gesi ya Oryx wakati wa hafla ya ugawaji wa mitungi 700 ya kupikia ya Oryx kwa baba lishe na mama lishe Machi 13, 2024 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Visiwani Zanzibar.
Meneja Masoko Msaidizi wa Kampuni ya Gesi ya Oryx Angela Bitungwa akitoa elimu ya matumizi ya mtungi wa kupikia wa gesi ya Oryx wakati wa hafla ya ugawaji wa mitungi 700 ya kupikia ya Oryx kwa baba lishe na mama lishe Machi 13, 2024 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Visiwani Zanzibar.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages