Breaking

Monday, 25 March 2024

TGNP YAWANOA MABINTI WA VYUO MBALIMBALI KUONGEZA IDADI YA WANAWAKE VIONGOZI

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

MILA na desturi zenye mtazamo hasi pamoja na mzigo wa majukumu ya familia anayokabiliana nayo mtoto wa kike ikiwa ni kulea familia, kupika,kukusanya kuni na kuchota maji katika umbali mrefu, unamnyima nafasi ya kuwa mbunifu na kusimama katika nafasi mbalimbali za uongozi.

Hayo ameyasema leo Machi 25,2024 Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi.Lilian Liundi katika Mafunzo ya Jukwaa la wasichana (Young Feminist Forum) ikijumuisha wanafunzi wasichana kutoka vyuo vikuu ,ambapo ameeleza dhumuni la mafunzo hayo ni kuwanoa mabinti katika harakati za kuongeza idadi ya wanawake viongozi.

Amesema kuwa katika Mafunzo hayo wasichana waliowahi kupitia katika nyanja mbalimbali za uongozi watazungumza kutoa uzoefu wao kwa lengo la kuhamasisha wengine ambao bado hawajapitia ili nao wathubutu kujishirikisha na jambo hilo.

"Hawa wakimaliza vyuo ndio wanaenda kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wameshaonesha nia na uwezo,kwamba wanaweza kuwa viongozi kwahiyo hiyo nikama kuwataarisha ili kuwaandaa wabunge watarajiwa,mawaziri watarajiwa hata,Marais"Bi.Lilian amesema.

Aidha Bi.Lilian amesema ingawa vijana ni wengi hasa watoto wa kike chakushangaza uwakilishi katika vyombo vya maamuzi ni hafifu au hakuna, jambo ambalo linachangia kudumaa kwa maendeleo ya nchi kwa kundi hili kuachwa nyuma.

"Ukiangalia bungeni tunaangalia tu asilimia 37 ni wanawake lakini ndani ya hao vijana ni wangapi,ndani ya bunge Zima vijana ni wangapi,na tunaangalia vijana ambao hawana miaka zaidi ya 35 sababu watu wenye miaka 40 au 50 tukiwaita ni vijana sio sahihi"Amesema.

Kwa upande wake rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS),Bi.Vanessa Lutabana amesema kuwa hakuna usawa katika udahili wa wanafunzi chuoni ambapo asilimia 33.7 ni wanawake waliodahiliwa katika chuo chao jambo ambalo linawapa changamoto wanawake kugombea katika nafasi za uongozi.

Nae, rais mstaafu Chuo Kikuu Mzumbe Bi.Akila Boniphace ameeleza kuwa bado jamii haikubaliani na wanawake kuwa viongozi ambapo amesema uongozi hauangalii jinsia ila ni akili busara,maamuzi pamoja na misimamo.

"Serikali iendelee kutoa elimu kwa jamii kwasababu bado tamaduni zinaturudisha nyuma,zinaamini wanaume ndio wanaweza,lakini vijana wakike tunaweza sana majumu ambayo mwanaume anayafanya na pengine tunaweza kuyafanya zaidi"Bi.Akila ameeleza.

Mafunzo hayo yanafanyika kwa siku tatu kuanzia Machi 25-27,2024 ambapo yamehudhiriwa na vyuo mbalimbali baadhi ni wanafunzi kutoka chuo Kikuu Cha Dar es Salaam,Ardhi,IFM,Chuo Cha maji, UDOM,Pamoja na Chuo Cha Mipango.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi.Lilian Liundi akifungua Mafunzo kwa Jukwaa la wasichana (Young Feminist Forum) ikijumuisha wanafunzi wasichana kutoka vyuo vikuu kuhusu masuala ya uongozi. Mafunzo hayo ya siku tatu yamefunguliwa leo Machi 25,2024 katika Ofisi za TGNP Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi.Lilian Liundi akizungumza jambo wakati akifungua Mafunzo kwa Jukwaa la wasichana (Young Feminist Forum) ikijumuisha wanafunzi wasichana kutoka vyuo vikuu kuhusu masuala ya uongozi. Mafunzo hayo ya siku tatu yamefunguliwa leo Machi 25,2024 katika Ofisi za TGNP Jijini Dar es Salaam

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages