Breaking

Thursday, 7 March 2024

MBUNGE SANTIEL KIRUMBA AONGOZA MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE MSALALA, AGAWA TAULO ZA KIKE, SHUKA ZAHANATI YA BULIGE, SUKARI KWA WAJANE

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba ameongoza wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani huku akigawa taulo za kike na madaftari kwa watoto wanaotoka katika mazingira magumu, kugawa  sabuni na sukari kwa wanawake wajane katika kata ya Bulige na shuka 20  katika zahanati ya Bulige ambayo zilizopokelewa na mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Khamis Katimba na wauguzi wa zahanati hiyo.

Maadhimisho hayo yamefanyika Machi 6,2024 katika Kata ya Bulige ambapo Mhe. Santiel ametumia fursa hiyo kuwashauri wanawake kujitokeza kuwania nafasi za uongozi na kushiriki katika ngazi za maamuzi.

"Tunaelekea katika uchaguzi wa Serikali za mitaa, naomba wanawake mjitokeze kwa wingi kuwania nafasi za uongozi lakini pia niwasihi wanaume watuunge mkono ili kuhakikisha tunafikia usawa wa kijinsia kwa asilimia 50 kwa 50",amesema.

"Tukitumia falsafa ya 4R za Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ni rahisi kufikia kauli mbiu ya 'Wekeza kwa Wanawake: Kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii", ameongeza Mhe. Santiel.

Aidha amemshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta fedha nyingi kwa ajiki ya miradi ya maendeleo mkoani Shinyanga na kwa upande wa kata ya Bulige tayari serikali imepeleka huduma ya umeme na maji pamoja na ujenzi wa zahanati ya Bulige.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani katika Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba akiwa  na wanafunzi wameshikilia taulo za kike



Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages