Na Mwandishi Wetu
WAIMBAJI maarufu nchini kutoka Gethsemane Group Kinondoni (GGK)SDA wameachia video ya wimbo wao mpya unaoitwa Bwana Wastahili.
Video ya wimbo huo imeachiwa leo Machi 18,2024 saa mbili usiku na imerekodiwa katika Studio ya Flying Wave Studio na kuongozwa na Director maarufu ajulikanae kama Director Joowzey.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya video hiyo kuachiwa hewani(kuzinduliwa) Mwenyekiti wa Gethsemane Group Kinondoni GGK Geoffrey Joseph amesema ni furaha kwao kuja na video ya wimbo huo ambayo imebeba ujumbe wa kumuabudu na kumtukuza Mungu.
"Ujumbe mkubwa kwenye wimbo huu ni kwamba Mungu pekee ndie anastahili kuabudiwa na yeye ndiye anatosha kwa kila kitu hasa kipindi hiki ambacho baadhi ya madhehebu wapo Kwenye mfungo, tunaamini wimbo huu ni ibada na utawasogeza karibu zaidi na Mungu,"amesema Joseph