Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Uhuru Fm, Bi. Amina Aziz wakati akitembezwa maeneo mbalimbali ya redio hiyo, kujionea inavyofanya kazi, wakati alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea vyombo vya habari vya African Media Group Limited (AMGL), Uhuru Publications Limited (UPL), Uhuru Fm na Uhuru Media Group (UMG) leo Alhamis, Machi 7, 2024, jijini Dar Es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi akisalimiana naa baadhi ya watangaji wa Radio Magic Fm, waliokuwa chumba cha kutangazia, alipofanya ziara katika Ofisi za Africa Media Group Limited, kujionea namna vyombo hivyo vinavyofanya kazi ya kuhabarisha, kuburudisha na kuelimisha umma, ikiwa ni sehemu ya ziara yake, ambayo pia ilimfikisha Uhuru Publications Limited (UPL) Uhuru FM na Uhuru Media Group (UMG) kujionea vinavyofanya kazi, leo Alhamis, Machi 7, 2024, jijini Dar Es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi akizungumza na watumishi wa Vyombo vya Habari vya Africa Media Group Limited (AMGL), Uhuru Publications Limited (UPL) Uhuru Fm na Uhuru Media Group (UMG) baada ya ziara ya kuvizungukia vyombo hivyo na kujionea utendaji kazi wake, leo Alhamis, Machi 7, 2024, jijini Dar Es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi akipata maelezo kutoka kwa Uongozi wa Uhuru Publications Limited, jinsi chombo hicho cha habari kinavyotekeleza majukumu yake. Kutoka kulia pichani ni Kaimu Mhariri Mtendaji wa Uhuru, Ndugu Ramadhani Mkoma, Mkuu wa Idara ya Itikadi, Uenezi, na Mafunzo wa CCM, Ndugu Paul Makonda, Mkurugenzi Mkuu wa Vyombo vya Habari vya CCM, Ndugu Shaaban Kissu, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi, Ndugu Dunia Mibavu, Kaimu Meneja wa Utawala, Ndugu Uwezo Kasongo, na Kaimu Meneja Biashara, Elisante Mzengi. Balozi Dk. Nchimbi alitembelea UPL, wakati akiwa alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea vyombo vya habari vya African Media Group Limited (AMGL), Uhuru Publications Limited (UPL), Uhuru Fm, na Uhuru Media Group (UMG) leo Alhamis, Machi 7, 2024, jijini Dar Es Salaam.