RAIS Mstaafu wa Awamu ya nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita katika juhudi zake za kuboresha Sekta ya Elimu nchini.
Akizungumza katika Hafla ya Uzinduzi wa Programu ya kuboresha Kada ya Ualimu (GPE TSP) Dk. Jakaya Kikwete amesema kwakushirikiana na Mfuko wa uendelezaji wa Sekta Elimu Duniani GPE mfuko huo umeweza kuendeleza Sekta ya Elimu nchini.
"GPE ni mfuko mkubwa wa kuendeleza Elimu bora katika nchi zinazo Endelea"Alisema Dk Kikwete.
Dk .KiKwete aliongeza kuwa lengo la Mpango wa GPE nikuhakikisha kila mtoto barani Afrika anapata fursa ya kupata Elimu.
Alisisitiza kuwa Miongoni mwanchi wananachama wa Mpango huo wa GPE 89 kati hizo nchi 44 zipo chini ya mpango huo wa maboresho ya sekta ya Elimu ambazo zipo katika bara la Afrika.
Naye Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Aldof Mkenda amesema Progamu ya uboreshwaji wa kada ya ualimu inaendana na Mazingira wezeshi ya walimu.
Alisema katika kuleta Mageuzi ya Elimu nchini wizara yake inaangalia utoshelevu wa walimu sambamba uboreshwaji wa mitala ya Elimu sambamba na Vitendea kazi.