Zoezi hilo linaendelea kutekelezwa ambapo mita 140 zimekaguliwa katika maeneo ya Masaki, Mkwajuni, Msasani, Coco beach, Victoria, Mikocheni, Block 41 na Mwananyamala.
Lengo la ukaguzi wa dira za maji wa mara kwa mara ni kuhakikisha ufanisi mzuri wa mita hizo, kudhibiti upotevu wa maji pamoja na kurahisisha usomaji wa mita kwa mteja na watumishi wa DAWASA.






