Breaking

Tuesday, 27 February 2024

RC MNDEME KUFANYA ZIARA YA KUSIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza na waandishi wa habari

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme anatarajia kufanya ziara ya kusikiliza kero na changamoto za wananchi na kuzitatua katika Manispaa ya Shinyanga, Kahama na Halmashauri ya Msalala kuanzia Februari 28 hadi Machi 1,2024.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumanne Februari 27,2024, Mhe. Mndeme amesema Februari 28,2024 atasikiliza kero za wananchi Soko Kuu ,kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga kuanzia saa tano asubuhi.


"Februari 29,2024 kuanzia saa tano asubuhi nitasikiliza kero za wananchi katika kata ya Majengo Manispaa ya Kahama. Machi 1,2024 nitakuwa Kata ya Kakola Halmashauri ya Msalala na kuanzia saa nane mchana siku hiyo nitafanya mkutano wa hadhara katika kata ya Segese Halmashauri ya Msalala", amesema Mhe. Mndeme.

"Karibuni sana wananchi wote, tupo tayari kupokea kero na changamoto na kuzifanyia kazi lakini pia tupo tayari kupokea maoni ya wananchi", ameongeza Mkuu wa Mkoa

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza na waandishi wa habari
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza na waandishi wa habari
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages