Ubalozi wa Qatar Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Qatar Charity, kwa niaba ya Serikali ya Qatar, umewasilisha misaada muhimu ya kibinadamu kwa waathirika wa Maporomoko ya Udongo yaliyotokea Hanang mkoani Manyara.
Shehena ya misaada hiyo iliyotolewa leo tarehe 18 Februari 2024 kwa kutumia ndege mbili za mizigo kutoka Qatar inalenga kugusa maisha ya wananchi wa Hanang walioathirika na maafa hayo ambayo madhara yake yalikuwa makubwa.
Serikali ya Qatar imetoa kwa ukarimu misaada hiyo ya kibinadamu inayojumuisha chakula kikavu katika vifungashio 1,440 (Dry food basket), chakula kilicho tayari kuliwa katika vifungashio 3,024 (Ready to Eat canned food) na vifaa vya usafi wa wanawake jumla 4,200 (women’s dignity kit) na hivyo kufanya jumla ya tani 90 za shehena.
Naye Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga amesema kuwa Serikali imepokea kwa moyo wa upendo misaada hiyo itakayoleta faraja kwa Waathirika na kuahidi kufikishwa kwa Walengwa kama ilivyokusudiwa.
Vilevile Mhe. Nderiananga ameeleza kuwa Serikali inatambua mchango wa wadau wote ikiwemo wananchi, sekta binafsi, asasi za kiraia na kidini, mashirika ya kimataifa na umoja wa mataifa kwa ushiriki wao katika kusaidia wananchi walioathirika na maporomoko ya tope katika wilaya ya
Akipokea Misaada hiyo Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe Queen Cuthbert Sendiga ameishukuru Serikali ya Qatar kupitia Qatar Charity kwa misaada hiyo ya kibinadamu ambayo itakwenda kuwasaidia wananchi wa Hanang kurejea kwenye hali yao ya Kawaida.
Aidha, Mhe Mkuu wa Mkoa amesema kuwa kupatikana kwa Misaada hiyo ni matokeo ya mahusiano mazuri ya nchi ya Tanzania na nchi za jirani ambayo yameimarishwa na serikali ya awamu ya sita Chini Rais Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Viongozi waliohudhuria hafla hiyo fupi iliyofanyika katika uwanja wa ndege wa KIA.