Breaking

Thursday, 22 February 2024

MANISPAA YA SHINYANGA YAZINDUA RASMI, PROGRAMU YA PJT MMMAM

Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Elizabeth Mweyo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu Jumuishi ya Malezi na Makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto (PJT MMMAM) katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga 
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Aaron Laizer (katikati) akizindua Programu Jumuishi ya Malezi na Makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto (PJT MMMAM) katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga leo Alhamisi Februari 22,2024. Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Mwalimu Alexius Kagunze. Kushoto ni Kaimu Mganga Mkuu Manispaa ya Shinyanga, Charles Malogi

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Jamii imetakiwa kuwekeza nguvu katika malezi na makuzi ya mtoto kwa sababu kundi la watoto wadogo linahitaji kuangaliwa kwa karibu na kufanyiwa uwezeshaji ili waweze kuwa rasilimali bora yenye tija kwa familia na taifa.

Rai hiyo imetolewa leo Alhamisi Februari 22,2024 na Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Aaron Laizer ambaye ni Afisa Tarafa Samuye wakati akizindua Programu Jumuishi ya Malezi na Makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto (PJT MMMAM) katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

Laizer amesema lengo la uanzishwaji wa Programu hiyo, ambayo kwa mkoa wa Shinyanga inatekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na Shirika lisilo la kiserikali la Iinvesting In Children and Strengtherning Their Societies (ICS) ni kuwa na uwekezaji unaoratibiwa kwenye maeneo matano ya mfumo wa malezi jumuishi ambayo ni Afya bora,Lishe, malezi yenye mwitikio, fursa za ujifunzaji wa awali na ulinzi na usalama.

“Serikali ilizindua Programu ya PJT MMMAM mwezi Desemba 2021,hapa katika Manispaa ya Shinyanga tumezindua rasmi leo. Kwa mujibu wa takwimu za taifa, Tanzania ina takribani watoto 16,524,201 wenye umri kati ya miaka 0-8 ambayo ni asilimia 30 ya watu wote. Hii ina maanisha kuwa katika kila watu watatu, kuna mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 0-8”,amesema.

“Programu hii itaongeza kasi ya mafanikio yanayopatikana katika malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto kwa kuimarisha ushirikiano wa wadau wa sekta mbalimbali katika utoaji wa huduma za malezi jumuishi kwa mtoto”,ameongeza Laizer.

Amesema uwekezaji katika huduma za MMMAM huwasaidia watoto kufikia upeo wao wa ukuaji timilifu lakini pia unalea faida kiuchumi.

Mratibu wa Elimu ya Afya kwa umma Mkoa wa Shinyanga, Moses Mwita, ameeleza kuwa, Malezi ,makuzi na maendeleo ya mtoto ni hatua jumuishi zenye muunganiko wa vipengele vyote vya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto katika ukuaji wa mwili, akili,lugha,kijamii,kitamaduni, kihisia na kimaadili.

“Ushahidi wa kisayansi unaonesha ni muhimu kuwekeza mapema kwa mtoto kwa kuwa ukuaji unaanza wakati wa kutungwa kwa mimba hadi miaka nane ambacho ni kipindi cha ukuaji zaidi. Kipindi hiki cha ukuaji na ujifunzaji huchukua nafasi kiasi kikubwa na ni kipindi ambacho ni msingi wa maisha ya mtoto unaochukua nafasi kiakili, kimwili, kijamii na kihisia”,ameeleza Mwita.

“Ubongo huanza kukua kabla hatujazaliwa,miaka 0-8 ukuaji na ujifunzaji wa watoto kwanza hutokea kupitia milango yao ya fahamu. Ujifunzaji wa watoto hutokea wakati watoto wanapocheza. Kila dakika unayochangamana na mtoto husaidia ukuaji wa ubongo”,amefafanua.

Amevitaja vitu vya msingi katika malezi ya mtoto kuwa ni lishe bora, kucheza, kupumzika, maji safi na salama ya kunywa, afya bora, ulinzi na usalama wa mtoto, uchangamshi wa awali na vifaa vya michezo.

“Vihatarishi vinavyosababisha mtoto kutofikia ukuaji timilifu ni umaskini, lishe duni, kumnyima fursa ya kucheza, ukatili, kukosa chanjo muhimu, msongo wa mawazo wa familia,utapiamlo, msongo wa mawazo wakati wa ujauzito, kukosa malezi yenye mwitikio na wazazi kutojali mahitaji ya watoto kwa wakati”,ameongeza.

Amesema ukuaji wa mtoto unahitaji sana huduma jumuishi ambazo ni afya bora, lishe toshelezi, malezi yenye mwitikio, fursa za ujifunzaji wa awali na ulinzi na usalama.

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vituo vya kulelea watoto (Day Cares) Wilaya ya Shinyanga , Damary Mollessi amesema vituo hivyo vinasimamia malezi na makuzi ya watoto kwa sababu wanakaa na watoto muda mrefu hivyo watahakikisha wanasimamia na kutekeleza kikamilifu Programu hiyo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la wazee Manispaa ya Shinyanga, Stephano Tano amewataka wazazi kuwajibika kwa kuhakikisha wanawapa chakula shuleni ili wakue vizuri.

“Hii Programu ni nzuri sana katika makuzi ya mtoto, naomba tuchukulie kwa uzito jambo hili ili kumjenga mtoto. Hawa wazazi legelege wanaouzuia watoto wasipate chakula shuleni tuwachukulie hatua. Hii ni roho mbaya kuwanyima chakula watoto shuleni, huu ni ukatili, wewe unakula nyumbani mtoto anashinda na njaa shuleni, tuwapeni watoto chakula shuleni”,amesema Tano.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Aaron Laizer (katikati) akizindua Programu Jumuishi ya Malezi na Makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto (PJT MMMAM) katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga leo Alhamisi Februari 22,2024. Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Mwalimu Alexius Kagunze. Kushoto ni Kaimu Mganga Mkuu Manispaa ya Shinyanga, Charles Malogi

Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Aaron Laizer akizungumza wakati akizindua Programu Jumuishi ya Malezi na Makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto (PJT MMMAM) katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga 

Kaimu Mganga Mkuu Manispaa ya Shinyanga, Charles Malogi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu Jumuishi ya Malezi na Makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto (PJT MMMAM) katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga 
Kaimu Mganga Mkuu Manispaa ya Shinyanga, Charles Malogi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu Jumuishi ya Malezi na Makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto (PJT MMMAM) katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga 
Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Elizabeth Mweyo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu Jumuishi ya Malezi na Makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto (PJT MMMAM) katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga 
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga, Lydia Kwesigabo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu Jumuishi ya Malezi na Makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto (PJT MMMAM) katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga 

Mratibu wa Elimu ya Afya kwa umma Mkoa wa Shinyanga, Moses Mwita akielezea kuhusu Programu Jumuishi ya Malezi na Makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto (PJT MMMAM)

Wadau wakiwa ukumbini wakati wa uzinduzi wa Programu Jumuishi ya Malezi na Makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto (PJT MMMAM)

Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vituo vya kulelea watoto (Day Cares) Wilaya ya Shinyanga , Damary Mollessi akizungumza wakati wa uzinduzi wa PJT MMMAM Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la wazee Manispaa ya Shinyanga, Stephano Tano akizungumza wakati wa uzinduzi wa PJT MMMAM Manispaa ya Shinyanga
Mwakilishi wa Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS), Dkt. Temba Fidelis akizungumza wakati wa uzinduzi wa PJT MMMAM Manispaa ya Shinyanga
Wadau wakiwa ukumbini wakati wa uzinduzi wa Programu Jumuishi ya Malezi na Makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto (PJT MMMAM)
Wadau wakiwa ukumbini wakati wa uzinduzi wa PJT MMMAM
Afisa Elimu Watu wazima mkoa wa Shinyanga, Dedan Rutazika akizungumza wakati wa uzinduzi wa PJT MMMAM Manispaa ya Shinyanga
Wadau wakiwa ukumbini wakati wa uzinduzi wa Programu Jumuishi ya Malezi na Makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto (PJT MMMAM)
Wadau wakiwa ukumbini wakati wa uzinduzi wa PJT MMMAM
Wadau wakiwa ukumbini wakati wa uzinduzi wa PJT MMMAM
Wadau wakiwa ukumbini wakati wa uzinduzi wa PJT MMMAM
Wadau wakiwa ukumbini wakati wa uzinduzi wa PJT MMMAM
Wadau wakiwa ukumbini wakati wa uzinduzi wa PJT MMMAM
Wadau wakiwa ukumbini wakati wa uzinduzi wa PJT MMMAM
Wadau wakiwa ukumbini wakati wa uzinduzi wa PJT MMMAM
Wadau wakiwa ukumbini wakati wa uzinduzi wa PJT MMMAM
Wadau wakiwa ukumbini wakati wa uzinduzi wa PJT MMMAM
Wadau wakiwa ukumbini wakati wa uzinduzi wa PJT MMMAM
Wadau wakiwa ukumbini wakati wa uzinduzi wa PJT MMMAM
Wadau wakipiga picha ya kumbukumbu wakati wa uzinduzi wa PJT MMMAM

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages