Breaking

Tuesday, 6 February 2024

MAADHIMISHO YA KUTOKOMEZA UKEKETAJI TGNP YATUMIA BONANZA NA FILAMU.

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) imefanya maadhimisho ya kupinga vitendo vya Ukatili kwa kishindo yenye lengo la kutokomeza Ukeketaji 2024 kwa kutumia msafara wa basi za abiria kwenye vituo vya Mabibo, Buguruni,Banana,Kipunguni na Kivule.

Akizungumza na Mwandishi wetu Leo Februari 6,2024 Afisa kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania Katika Idara ya ujenzi nguvu za Pamoja na Harakati Bi.Flora Ndaba amesema wamejadiri mada mbalimbali kwenye basi hizo jinsi ya kuwekeza katika wanawake na kwa mabinti walionusurika kufanyiwa kitendo hicho.

Aidha amesema kuwa wametumia Bonanza na Sinema ambayo imeandaliwa na Mtandao huo wa jinsia kwa lengo la kupaza sauti zao kuujulisha Umma kuhusiana na Janga hilo la ukeketaji.

"Tupo kwenye Soko la Kivule na hapa Kuna tupo na wadau ambapokuna Sinema ambayo imeandaliwa na TGNP pamoja na ufadhili wa Umoja wa Mataifa"Bi.Flora amesema.

Kwa Upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Bi.Magdalena Msaki ameeleza kuwa wamejipanga kuzuia kitendo hicho cha ambapo amebainisha kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto Ukeketaji ni kosa la Jinai.

"Kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 na iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019 ukeketaji ni kosa la jinai kwahiyo tunataka kutoa Elimu kwa jamii inayotuzunguka katika kata hizi tatu"Bi Magdalena amesema

Nae mwanaharakati wa jinsia Bw.Seleman Bishangazi amesema wameamua kushirikisha Vijana kwa madhumuni ya kupaza sauti zao jamii itambue ni jambo baya na kuachana na jambo hilo.

Maadhimisho hayo yamebeba Kauli mbiu isemayo Sauti yangu,Hatma yangu ambapo yamefanyika kwa mkoa wa Dar es Salaam katika Wilaya ya Ilala ambayo imethibitika kuwa ni kinara wa ukatili huo.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages