Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mhe. Patrobas Katambi (katikati) ambaye ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu akiendesha gari la kubebea wagonjwa ‘Ambulance’ ajili ya Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mhe. Patrobas Katambi (katikati) ambaye ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu akikata utepe wakati akikabidhi gari la kubebea wagonjwa ‘Ambulance’ ajili ya Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu amekabidhi gari maalumu la kubebea wagonjwa ‘ Ambulance’ na Vitanda 8 kwa ajili ya wagonjwa katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga pamoja na majiko 145 ya gesi kwa makundi mbalimbali ya jamii.
Akizungumza wakati wa kukabidhi gari, vitanda na majiko ya gesi leo Alhamisi Februari 8,2024 katika Stendi ya magari ya Kambarage, Mhe. Katambi amesema gari hilo pamoja na vitanda vitasaidia wananchi katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
“Nimekuja kukabidhi gari hili ‘Ambulance’ niliyopewa na Mama, Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ili lisaidie kuboresha huduma za afya katika hospitali yetu ya Manispaa ya Shinyanga. Pia baada ya kutoa vitanda 17 leo nimeamua kuongeza vitanda vingine nane ili vikasaidie katika wodi zetu. Rais Samia anataka wananchi wapate huduma bora za afya”,ameeleza Katambi.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mhe. Patrobas Katambi (katikati) ambaye ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu akikabidhi gari la kubebea wagonjwa.
“Lakini pia bado ninaendelea na zoezi la kugawa majiko ya gesi kwa makundi mbalimbali yasaidie katika kutunza mazingiria ili kupambana na mabadiliko ya tabia nchi ambapo nakabidhi majiko 145 kwa ajili ya Wakuu wa Idara katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Mwenyekiti na Katibu wa Chama cha Walimu Manispaa ya Shinyanga,Maafisa tarafa, watendaji wa kata, shule za sekondari na msingi na Hospitali za Manispaa ya Shinyanga”,ameongeza Mhe. Katambi.
Katika hatua nyingine Katambi amesema serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya afya, elimu, barabara na ujenzi wa masoko.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Revocatus Lutundu amemshukuru Mbunge Katambi kwa kushughulikia haraka changamoto ya gari la wagonjwa.
“Tulikuwa na changamoto ya gari la wagonjwa katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga, baada ya kumwelezea Mbunge kuhusu changamoto hii, kaifanyia kazi na leo tunapokea gari hili. Tutaendelea kumpa ushirikiano kwani amekuwa msaada mkubwa katika mambo mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa miradi. Mambo meng yamewezekana kutokana na mkono wa Mbunge Katambi”,amesema Lutundu.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Dkt. Elisha Robert amesema gari hilo ni zuri litasaidia kuokoa maisha ya mama na mtoto.
“Tumekuwa na changamoto ya magari ya wagonjwa. Tulikuwa na magari mawili, moja likapata hitilafu,tukabaki na moja ambalo pia lina changamoto, hivyo tumekuwa tukilazimika kutumia gari la utawala kama Ambulance sasa baada ya kupata gari hili ‘Mnyama huyu’ mambo yatakuwa mazuri licha ya kwamba bado tunahitaji magari zaidi”,amesema Dkt. Robert.
Nao Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Odiria Batimayo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Anord Makombe na Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Elias Masumbuko wamesema gari hilo la wagonjwa litasaidia kupunguza changamoto ya usafiri kwa wagonjwa lakini pia vitanda vitasaidia wagonjwa wodini ikiwa ni matunda mazuri yanayotokana na Uongozi mzuri wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu akizungumza leo Alhamis Februari 8, 2024 wakati akikabidhi gari maalumu la kubebea wagonjwa ‘Ambulance’ na Vitanda 8 kwa ajili ya wagonjwa katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga pamoja na majiko 136 ya gesi kwa makundi mbalimbali ya jamii. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu akizungumza akikabidhi gari la kubebea wagonjwa ‘Ambulance’ na Vitanda 8 kwa ajili ya wagonjwa katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga pamoja na majiko 136 ya gesi kwa makundi mbalimbali ya jamii.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu akizungumza akikabidhi gari la kubebea wagonjwa ‘Ambulance’ na Vitanda 8 kwa ajili ya wagonjwa katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga pamoja na majiko 136 ya gesi kwa makundi mbalimbali ya jamii.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mhe. Patrobas Katambi (katikati) ambaye ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu akikata utepe wakati akikabidhi gari la kubebea wagonjwa ‘Ambulance’ ajili ya Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mhe. Patrobas Katambi (katikati) ambaye ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu baada ya kukata utepe wakati akikabidhi gari la kubebea wagonjwa ‘Ambulance’ ajili ya Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mhe. Patrobas Katambi (katikati) ambaye ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu akiwa ndani ya gari la kubebea wagonjwa ‘Ambulance’ ajili ya Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Anord Makombe
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mhe. Patrobas Katambi (katikati) ambaye ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu akiwa ndani ya gari la kubebea wagonjwa ‘Ambulance’ ajili ya Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Anord Makombe
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mhe. Patrobas Katambi (katikati) ambaye ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu akiendesha gari la kubebea wagonjwa ‘Ambulance’ ajili ya Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Muonekano wa gari la kubebea wagonjwa ‘Ambulance’ ajili ya Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Muonekano wa gari la kubebea wagonjwa ‘Ambulance’ ajili ya Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Muonekano wa vitanda na gari la kubebea wagonjwa ‘Ambulance’ ajili ya Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mhe. Patrobas Katambi (kulia) ambaye ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Revocatus Lutundu vitanda 8 ajili ya Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mhe. Patrobas Katambi (katikati) ambaye ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Revocatus Lutundu (kushoto) vitanda 8 ajili ya Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga. Kulia ni Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Odiria Batimayo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Odiria Batimayo (katikati) na viongozi mbalimbali wakifurahia jambo wakati wa makabidhiano ya vitanda vya hospitali
Muonekano wa majiko ya gesi, moja ya vitanda na gari la wagonjwa
Muonekano wa majiko ya gesi yaliyotolewa na Mbunge Patrobas Katambi
Muonekano wa majiko ya gesi yaliyotolewa na Mbunge Patrobas Katambi
Muonekano wa majiko ya gesi yaliyotolewa na Mbunge Patrobas Katambi
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu akiendelea na zoezi la kukabidhi majiko kwa makundi mbalimbali ya jamii

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Revocatus Lutundu akizungumza wakati wa hafla hiyo
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Odiria Batimayo akizungumza wakati wa hafla hiyo
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Anord Makombe akizungumza wakati wa hafla hiyo
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Dkt. Elisha Robert akizungumza
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu akisalimiana na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Dkt. Elisha Robert (kulia).