Breaking

Thursday 29 February 2024

BREAKING: RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI AFARIKI DUNIA





Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi aliyefariki Dunia leo Februry 29,2024 saa
11:30 Jioni katika Hospitali Jijini Dar es salaam alipokuwa
akipatiwa matibabu kwa ya ugonjwa wa Saratani ya
Mapafu.

Rais Samia amesema Mzee Mwinyi alikuwa
akipatiwa matibabu tangu November 2023 London
Uingereza na baadaye kurejea Nchini na kuendelea na
matibabu Mzena Hospital.


Aidha Rais Samia ametangaza siku saba za maombolezo kuanzia kesho ijumaa March 01, 2024.

Ali Hassan Mwinyi alikuwa Rais wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania kuanzia mwaka 1985 hadi 1995.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages