NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (Sayansi) Prof.James Mdoe ametembelea na kukagua ujenzi wa Kituo cha kufundishia Umahiri wa Tehama katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) ambacho kitatengeneza wataalamu katika masuala ya ujenzi wa Teknolojia.
Ujenzi wa Kituo hicho kikubwa nchini unadhaminiwa na Benki kuu ya dunia (WB).
Akizungumza mara baada ya kutembelea mradi huo leo Januari 29,2024 Jijini Dar es Salaam, Prof. Mdoe amewataka mkandarasi kuongeza watendaji kazi kwa lengo la kusaidia kazi kukamilika kwa wakati ili kuruhusu majengo hayo yaanze kutumika katika mtaala mpya wa kujenga umahiri katika fani hizo.
Aidha ameeleza kuwa majengo ambayo yanajengwa yananafasi kubwa ya kubeba watafiti ambao watahitaji kufanya tafiti katika chuo hicho ambapo amesema kuwa taasisi hiyo Ina mashirikiano na watu wengi.
Pamoja na hayo amesema kuwa katika kituo hicho kitakuwa na maabara ambazo zinahusiana na kutengeneza roboti, kujifunza masuala ya akili bandia (artificial intelligence) na mambo ya mtandao.
"Tunatengenza maabara Kuna watu watakuja kutengeneza maroboti,watajifunza masuala ya akili bandia,masula ya mtandao,,ujenzi huu ulitakiwa ukamilike februari Sasa wameongezewa miezi miwili kwenye jengo hili na la bweni". Amesema Prof. Mdoe.
Ujenzi huo unakadiriwa hadi kukamilika kwake utatumia Bilioni 21.9 katika mradi huo ambao umelenga kuleta mapinduzi makubwa ya kidigiti nchini kwa kuzalisha wahitimu wenye Umahiri wa Tehama.