Breaking

Sunday, 28 January 2024

ORYX KUFUNGA MFUMO WA GESI MINAKI SEKONDARI, YAKABIDHI MITUNGU YA GESI 700 KISARAWE

Na Mwandishi Wetu

SHULE ya Sekondari Minaki mkoani Pwani inatarajiwa kufungiwa mfumo wa gesi na Kampuni ya Oryx Gas, kwa lengo la kuiwezesha kutumia nishati safi ya kupikia na kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa.

Pia Oryx kwa kushirikiana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makumu wa Rais Muungano na Mazingira Dk. Seleman Jafo,wamekabidhi mitungi 700 ya gesi kwa walimu 500 Wilaya ya Kisarawre Mkoani Pwani, pamoja na baba na mama lishe 200 ambayo inathamani ya zaidi ya shilingi milioni 50 .

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi hiyo kwa walimu wa shule za msingi na sekondari Wilayani humo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Benoit Araman alimshukuru Waziri Jafo, kwa kumpatia nafasi ya kupeleka nishati safi ya kupikia kwa walimu pamoja na Baba na Mama lishe wilayani Kisarawe.

“Oryx Gas tunaamini kwamba ukipika kwa kutumia gesi, inaleta maendeleo mengi kwa jamii yetu. Kupika kwa gesi ya Oryx ni kulinda mazingira kwa kuacha kukata miti. Zaidi ya yote ni kulinda afya ya wanawake kwa kuwaepusha kuvuta moshi na mvuke unaoathiri mapafu na afya yao unaotokana na kuni na mkaa.,”

“Wanawake wanatumia muda mchache kupika hivyo wanapata nafasi kufanya shughuli nyingine za maendeleo na kuepuka kugombana na wenza wao kwa kuchelewesha chakula, na wanaume pia watajiongezea marks ukiwazadia wamama mitungi ya gesi.Kwa kutumia gesi ya Oryx, Watoto wanakua na muda mwingi zaidi kusoma na sio kwenda kutafuta kuni.”

Amesisitiza kuwa kuanzia Julai mwaka 2021 wamekuwa mstari wa mbele kutekeleza maelekezo ya Serikali waliyopokea kutoka kwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kuwa ifikapo mwaka 2032 asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia.

Araman alisema Oryx Gas inataka kutokomeza matumizi ya nishati chafu ya kuni na mkaa ambayo si tu mbaya kwa afya bali pia ni hatari kwa mazingira.

Aliongeza kuwa, Oryx Gas inatekeleza juhudi za kueneza matumizi ya nishati safi kwa Watanzania wengi ipasavyo ambayo ni ndoto kubwa ya Rais Dk. Samia

Pia alisema Oryx Gas inatekeleza agizo la serikali kwa kuhakikisha taasisi zenye watu zaidi ya 100 , ikiwemo shule, kambi za jeshi, vyuo vya polisi, magereza zinatia nishati safi, kwa kutengeza mifumo salama ya gesi, ambayo itatumia tenki mifumo hiyo.

“Hii inasaidia kupunguza matumizi ya mafuta machafu kwenye mifumo ya uzalishaji. Oryx Gas Tanzania inajipongeza kwa kujulikana kua kampuni kinara katika usambazaji wa gesi ya kupikia majumbani kwa Watanzania kwa sasa. Sisi Oryx Gas Tanzania tutaendelea kuwekeza zaidi katika kuratibu kubadilisha na kueneza nishati safi kutumika na Watanzania kwa kutumia gesi ya Oryx kwa manufaa yetu wote.”

Pia amehimiza wananchi kutumia gesi ya LPG katika shughuli zao mbalimbali ili kuleta maendeleo katika nchi ya Tanzania na kwa ajili ya kuboresha Maisha yetu kiujumla huku akitumia nafasi hiyo kueleza Waziri Jafo amekuwa balozi mzuri wa kuleta maendeleo kwa waalimu na jamii kiujumla kwa kuunga mkono katika mpango huo wa matumizi ya nishati safi wilayani Kisarawe.

Akizungumzia kuhusu kufunga mfumo wa nishati safi ya kupikia katika Shule ya sekondari ya Minaki , Aramn, alisema mfumo huo utakua na uwezo wa kubeba ujazo wa tani moja ya gesi.

Kwa upande wake Waziri Jafo aliishukuru Oryx kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Rais Dk.Samia katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi kwa vitendo , huku akieleza kuwa tayari Serikali imeshatoa maelekezo kuanzia mwaka huu wa 2023 taasisi , mashirika na maeneo ambayo yana watu kuanzia 100 kuanza kutumia nishati safi ya kupikia ikiwemo nishati

Alisema mbali ya kugawa mitungi ya gesi kwa walimu 500, bado ataendelea kuzungumza na wadau, apate mitungi mingine kwani lengo lake ni kuhakikisha walimu wote 1300 walioko katika wilaya hiyo wawe wamepata mitungi ya gesi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Dk.Selemani Jafo(katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Bonoit Araman (kushoto) wakimkabidhi mtungi wa gesi ya Oryx Mwalimu wa Shule ya Msingi Chanzige B iliyopo Kisarawe mkoani Pwani Mariam Mhando (kulia) ikiwa ni sehemu ya mitungi 700 iloyotolewa na kampuni hiyo kwa ajili ya walimu 500 pamoja na Baba na Mama Lishe 200 katika Wilaya hiyo.
Waziri wa Nchi , Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dk.Selemani Jafo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Benoit Araman( kushoto) wakimkabidhi mtungi wa gesi ya Oryx Mwalimu Samida Msofe wakati wa hafla ya ugawaji mitungi ya gesi na majiko yake kwa walimu wa shule zilizopo wilayani Kisarawe mkoani Pwani
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Dk.Selemani Jafo akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi ya oryx 700 pamoja na majiko yake kwa walimu , Baba Lishe na Mama Lishe wilayani Kisarawe mkoani Pwani
Meneja Masoko wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Peter Ndomba akitoa elimu ya matumizi salama ya mtungi wa gesi kabla ya kukabidhiwa kwa walimu pamoja na baba na mama lishe wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani ambapo ametumia nafasi hiyo kusisitiza matumizi sahihi ya gesi ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea kwa mtumiaji
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages