NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
OFISI ya Waziri Mkuu imesaini hati mbili za Makubaliano (MOU) kati ya Mamlaka ya Uendelezaji wa Mji Mkuu wa Korea Kusini na Kampuni ya Usanifu Majengo ya HEERIM kuhusu Uendelezaji na Ujenzi wa Mji wa Serikali Dodoma.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo leo Januari 26,2024 Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama kusainiwa kwa Hati za Makubaliano kutaweka msingi wa imara wa biashara na uwekezaji kati ya nchi hizo mbili huku tukitarajia miradi mingi zaidi kutekelezwa nchini hususani Jijini Dodoma ambako ndiko yalipo makao makuu ya nchi.
Amesema ushirikiano uliopo kati ya nchi hizo umepelekea utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati likiwemo daraja maarufu la Tanzanite ambalo lilijengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Korea Kusini kupitia Mfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kiuchumi (Economic Development Cooperation Fund – EDCF).
Aidha amesema kuwa uhusiano huo umedhihirishwa pia na ziara za Viongozi wa ngazi ya juu katika Mataifa yetu haya mawili. Moja ya ziara hizo maalum ilifanywa Oktoba 2022 na Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye alifanya ziara ya kikazi nchini Korea Kusini.
"Akiwa Korea Kusini, Mheshimiwa Waziri Mkuu aliitembelea National Agency for Administrative City Construction, Taasisi hii ni Wakala wa Kitaifa Nchini Korea Kusini inayosimamia na kuendeleza ujenzi wa Jiji la Sejong, nchini humo. Kimsingi, Jiji la Sejong limejengwa kwa mandhari nzuri nay a kuvutia sana". Amesema
Pamoja na hayo Waziri Mhagama amesema maendeleo ya Jiji la Dodoma yanahitaji uwekezaji mkubwa katika majengo, maeneo ya mapumziko, mazingira, miundombinu ya mawasiliano na maeneo mengine ya kuvutia.
"Lengo hili litafikiwa kwa ufanisi endapo Serikali itaendelea kushirikiana na Sekta binafsi ili kufikia maendeleo haya. Kwa kuzingatia hilo, nitoe wito kwa Wawekezaji katika nyanja zote, wanaume kwa wanawake kuwekeza Jijini Dodoma ili kuuendeleza na kuupendezesha Mji wetu Mkuu". Ameeleza Waziri Mhagama.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa National Agency for Administrative City Construction Bw. Hyeong Ryeol Kim amesema utiaji saini wa makubaliano hayo ni fursa muhimu ya kuendeleza ushirikiano baina ya mataifa hayo.
Vilevile amesema watahakikisha uhusiano huo unadumu katika utekelezaji wa miundominu na mambo mengine.
Nae Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jimmy Yonaz amesema taifa la Korea Kusini imekua ikishirikiana na Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo Afya na Kilimo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama akishuhudia utiaji saini wa makubaliano kati ya Mamlaka ya Uendelezaji wa Mji Mkuu wa Korea Kusini na Kampuni ya Usanifu Majengo ya HEERIM na Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu Uendelezaji na Ujenzi wa Mji wa Serikali Dodoma. Wanaosaini ni Mtendaji Mkuu wa National Agency for Administrative City Construction Bw. Hyeong Ryeol KIM (kushoto) na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim James Yonaz. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 26,2024 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama akishuhudia utiaji saini wa makubaliano kati ya Mamlaka ya Uendelezaji wa Mji Mkuu wa Korea Kusini na Kampuni ya Usanifu Majengo ya HEERIM na Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu Uendelezaji na Ujenzi wa Mji wa Serikali Dodoma. Wanaosaini ni Mtendaji Mkuu wa National Agency for Administrative City Construction Bw. Hyeong Ryeol KIM (kushoto) na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim James Yonaz. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 26,2024 Jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa National Agency for Administrative City Construction Bw. Hyeong Ryeol KIM (kushoto) na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim James Yonaz wakionesha mikataba waliosaini kuhusu uendelezaji na ujenzi Mji wa Serikali Dodoma. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 26,2024 Jijini Dar es Salaam. Mtendaji Mkuu wa National Agency for Administrative City Construction Bw. Hyeong Ryeol KIM (kushoto) na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim James Yonaz wakibadilishana hata za mikataba waliosaini kuhusu uendelezaji na ujenzi Mji wa Serikali Dodoma. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 26,2024 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi zawadi Mtendaji Mkuu wa National Agency for Administrative City Construction Bw. Hyeong Ryeol KIM wakati wa utiaji saini wa makubaliano kati ya Mamlaka ya Uendelezaji wa Mji Mkuu wa Korea Kusini na Kampuni ya Usanifu Majengo ya HEERIM na Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu Uendelezaji na Ujenzi wa Mji wa Serikali Dodoma. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 26,2024 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi watendaji wa Serikali ya Tanzania pamoja na Maofisa wa National Agency for Administrative City Construction (NAACC) pamoja na Heerim Architects and Planners wakati wa hafla ya utiaji saini kati ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Mamlaka ya Uendelezaji wa Mji Mkuu wa Korea Kusini na Kampuni ya Usanifu Majengo ya HEERIM kuhusu Uendelezaji na Ujenzi wa Mji wa Serikali Dodoma. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 26,2024 Jijini Dar es Salaam Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja Mtendaji Mkuu wa National Agency for Administrative City Construction Bw. Hyeong Ryeol KIM na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim James Yonaz wakati wa hafla ya utiaji saini kati ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Mamlaka ya Uendelezaji wa Mji Mkuu wa Korea Kusini na Kampuni ya Usanifu Majengo ya HEERIM kuhusu Uendelezaji na Ujenzi wa Mji wa Serikali Dodoma. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 26,2024 Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama akipongezana na Mtendaji Mkuu wa National Agency for Administrative City Construction Bw. Hyeong Ryeol KIM
katika hafla ya utiaji saini kati ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Mamlaka ya Uendelezaji wa Mji Mkuu wa Korea Kusini na Kampuni ya Usanifu Majengo ya HEERIM kuhusu Uendelezaji na Ujenzi wa Mji wa Serikali Dodoma. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 26,2024 Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza katika hafla ya utiaji saini kati ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Mamlaka ya Uendelezaji wa Mji Mkuu wa Korea Kusini na Kampuni ya Usanifu Majengo ya HEERIM kuhusu Uendelezaji na Ujenzi wa Mji wa Serikali Dodoma. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 26,2024 Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim James Yonaz akizungumza katika hafla ya utiaji saini kati ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Mamlaka ya Uendelezaji wa Mji Mkuu wa Korea Kusini na Kampuni ya Usanifu Majengo ya HEERIM kuhusu Uendelezaji na Ujenzi wa Mji wa Serikali Dodoma. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 26,2024 Jijini Dar es Salaam
Mtendaji Mkuu wa National Agency for Administrative City Construction Bw. Hyeong Ryeol KIM akizungumza katika hafla ya utiaji saini kati ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Mamlaka ya Uendelezaji wa Mji Mkuu wa Korea Kusini na Kampuni ya Usanifu Majengo ya HEERIM kuhusu Uendelezaji na Ujenzi wa Mji wa Serikali Dodoma. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 26,2024 Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)