Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imekamilisha kazi ya ufungaji pampu mpya ya kusuma maji katika moja ya visima katika kata ua Kisarawe II kwa lengo la kuboresha huduma ya maji katika Viwanda na makazi ndani ya kata hiyo.
Akizungumzia utekelezaji wa kazi hiyo, Mhandisi wa mkoa wa kihuduma DAWASA Kigamboni Ndondole Ndondole , ameeleza kuwa kazi ya ufungaji wa pampu imekamilika na maeneo ya viwanda na wananchi watarajie huduma kuimarika katika eneo la Kisarawe II.
"Tumekamilisha ufungaji wa pampu na kazi nyingine zinaendelea ikiwa ni pamoja na maunganisho ya pampu kwenye mtandao wa usambazaji maji baada ya TANESCO kukamilisha kazi ya kufunga transformer" ameeleza mhandisi Ndondole.
Mhandisi Ndondole ameongeza kuwa kukamilika kwa kazi hiyo kutasaidia uboreshwaji wa huduma za maji kwa zaidi ya viwanda 6 na wananchi 477
Kwa upande wake ndugu Michael Gabriel mkazi wa Kisarawe II ameishukuru Serikali kwa utekelezaji kwa kazi hiyo na kuwataka watendaji DAWASA kuongeza nguvu zaidi ili ikamilike kwa wakati na kuleta matokeo chanya kwa jamii.
"Awali tulipata changamoto ya huduma kuwa sio ya kuridhisha hapo awali, huku baadhi ya maeneo yakipata maji kwa msukumo mdogo sana na mengine kukosa kabisa, ufungaji wa pampu hii tunategemea kuimarisha huduma na kumaliza changamoto zote zilizokuwepo hapo awali" ameeleza ndugu Michael.
Zoezi hili linatarajia kunufaisha wananchi takribani 500 wa maeneo ya mitaa ya Tumaini, Kichangani, na Kigogo pamoja na Viwanda vya Watercom drinking water, Kiwanda cha dawa (Dawason), Sitafill, Medical Dawlia Limited na Megapipe Limited.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990