Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) inaendelea na uboreshaji wa miundombinu ya huduma na kuhakikisha upatikanaji wa maji katika maeneo ya Kariakoo.
Akizunguzimia utekelezaji wa kazi hiyo Meneja wa DAWASA Mkoa wa kihuduma Ilala, Mhandisi Honest Makoi ameeleza kuwa zoezi linahusisha ubadilishaji wa bomba la inchi 6 kwa umbali wa zaidi ya mita 150 katika mtaa wa Livingstone pamoja bomba la inchi 4 kwa umbali wa zaidi ya mita 700 katika mtaa wa Kipata iliyoko eneo la Kariakoo.
"Mamlaka tumetumia fursa hii maboresho ya barabara kuwekwa katika kiwango cha lami na sisi kufanya maboresho ya miundombinu yetu ili tusaidie wananchi wa eneo la Kariakoo waliokuwa wanapata huduma ya maji kwa kasi ndogo kutokana miundombinu chakavu iliyokuwepo sasa wapate kwa kiwango bora zaidi" alisema Mhandisi Makoi.
Naye Mwenyekiti wa serikali ya mtaa Gerezani Mashariki, Ndugu Zainab Nketo ameeleza kuwa maboresho hayo ya miundombinu ya maji sio tu wanakwenda kusaidia kuongeza kasi ya upatikanaji wa huduma ya maji katika mitaa hiyo bali kuondoa kero ya muda mrefu ya uvujaji wa maji iliyokuwa ikipelekea uharibifu wa mara kwa mara ya miundombinu ya barabara.
"Kwanza nipongeze DAWASA walivyofanya maamuzi ya kuondoa hiyo miundombinu chakavu ya maji maana niya muda mrefu na yalikuwa inavuja mara kwa mara na kila muda ili tulazimu sisi viongozi kuwasumbua mafundi kuja kuziba maana wananchi wetu wanalalamika maji yanatoka kidogo kidogo majumbani kwao wakati mengine yanavuja tu barabarani" alisema Nketo.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990