Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Prof. Jamal Katundu ametembelea Mradi wa maji Kigamboni uliotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) na kusisitiza usimamizi dhabiti katika utekelezaji wa miradi ya maji pamoja na kuboresha upatikanaji wa huduma katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
Prof. Katundu ameyasema hayo wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji na kupokea taarifa juu ya utekelezaji wa Mradi wa maji Kigamboni uliokamilika.
"Nimeona juhudi za DAWASA katika kuboresha huduma ya maji katika Mkoa wa Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani, niwapongeze sana na niwasihi muendelee kusimamia kikamilifu miradi hii ili ilete faida kwa Serikali na wananchi wanaohudumiwa." amesema.
"Naamini kila mmoja ataenda kusimama kwa nafasi yake ili kufikia lengo la kumtua mama ndoo kichwani ifikapo mwaka 2025," ameeleza.
Kwa upande wake, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Ndugu Kiula Kingu ameeleza kuwa kazi kubwa imefanyika na inaendelea kufanyika katika usambazaji wa maji ili kuhakikisha yanawafikia wananchi wote.
"Tunaendelea kusimamia kwa karibu miradi ambayo imekamilika. Lakini tumepokea maelekezo ya Katibu Mkuu katika kusimamia kikamilifu miradi hii na kuendelea na usambazaji wa huduma ya maji kwa wananchi wote," ameeleza Ndugu Kingu.
Mradi wa maji Kigamboni unazalisha maji kiasi cha lita 70 umehusisha uendelezaji wa visima 7 na ujenzi wa tanki la milion 15 unahudumia Wananchi takribani 7300 katika wilaya ya Kigamboni na baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Ilala na Temeke.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990