Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi (katikati) akipalilia shamba na wananchi leo Januari 1,2024
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi (wa pili kulia) akiwa shambani na wananchi leo Januari 1,2024
TAZAMA KATAMBI AKIWA SHAMBANI KABAKI NA VEST TU
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi (kulia) akiwa kwenye kijiwe cha kahawa wananchi leo Januari 1,2024
***
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi amefungua mwaka mpya 2024 kwa kuibukia shambani na kupalilia mazao na wananchi wake wa kata ya Old Shinyanga ambapo amesisitiza wananchi hao kufanya kazi kwa bidii akimaanisha mwaka 2024 ni mwaka wa kazi.
“Nilikuwa nakwenda kuangalia miundombinu ya umeme niko na diwani wa Old Shinyanga nikaona nipite hapa naona mnapiga kazi tuendelee hivi hivi”, amesema Katambi.
Katambi yupo Jimboni Shinyanga Mjini kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii za kufunga 2023 na kuukaribisha mwaka 2024 ambapo ametembelea na kukagua ofisi mbili za CCM anazozijenga katika Kata za Ibadakuli na Chibe zitakazogharimu zaidi ya shilingi Mil.110 zitakapokamilika mpaka landscape na uzio. Pia anashiriki na kutoa mijadala na midahalo na semina kujadili maendeleo ya Jimbo lake na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa wananchi sokoni na Vijiwe vya Kahawa ambako amekutana na wananchi, viongozi wa dini, Bodaboda, Mama lishe, Wajasiriamali ambao wanaililia CCM wakisema apewe mitano tena na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.
Picha za matukio mbalimbali Mhe. Katambi akiwa Jimboni Shinyanga Mjini