Breaking

Saturday 13 January 2024

KAMPUNI YA ORYX YEPELEKA KICHEKO KWA BABA NA MAMA LISHE DODOMA MJINI

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

MAMA Lishe na Baba Lishe 500 kutoka katika Kata 41 za Jimbo la Dodoma Mjini wamepatiwa mitungi ya gesi ya Oryx pamoja na majiko yake lengo likiwa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia sambamba na kuwaepusha na madhara yanayotokana na nishati chafu ya kuni na mkaa kwa kuvuta moshi unaoharibu mapafu na hivyo kuleta madhara ya kiafya.

Wakizungumza leo wakati wa ugawaji wa mitungi hiyo ya gesi kwa Mama na Baba Lishe wa Dodoma Mjini, Mkurugenzi wa Kampuni ya Oryx Araman Benoit na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Waziri wa Nishati Athony Mavunde wamesema matumizi ya nishati safi ya kupika iliyotolewa kwa kundi hilo linakwenda kurahisisha shughuli zao za kila siku kwa kupika kwa muda mfupi kuliko wanapotumia kuni na mkaa.

Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Araman Benoite amesema mitungi 500 ya gesi ya oryx na majiko yake ambayo wameyetoa kwa mama na baba lishe hao ina thamani ya Sh.milioni 41 na kwamba wataendeela kufuata maelekezo ya serikali inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan inayohamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kuendeela kugawa mitungi hiyo kwa wananchi wa makundi mbalimbali.

Amesema Oryx Gas wanaamini kupika kwa gesi kunalinda mazingira kwa kuacha kukata kuni na mkaa lakini inalinda afya kwa kuwaepusha kuvuta moshi na mvuke unaoathiri mapafu na afya yao unaotokana na kuni na mkaa hivyo Baba na Mama Lishe ni kundi ambalo wanalipa kipaumbele kwa kutambua ndilo linatumia zaidi kuni na mkaa kila siku kwa shughuli zao za kuandaa chakula.

Pia amesema kwa kutumia nishati safi ya kupikia inayotokana na gesi wanawake wanatumia muda mchache kupika, hivyo wanapata nafasi kufanya shughuli nyingine za maendeleo na kuepuka kugombana na wenza wao kwa kuchelewesha chakula.

“Kuanzia Julai mwaka 2021 tumekuwa mstari wa mbele kutekeleza maelekezo ya Serikali tulioyapokea kutoka kwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuwa ifikapo mwaka 2023 asilimia 80 ya wananchi watumie nishati safi ya kupikia,” amesema na kusisitiza kupitia mipango hiyo, Oryx Gas inataka kutokomeza matumizi ya nishati chafu ya kuni na mkaa.


Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Athony Mavunde amesema wanashukuru kwa kupata majiko hayo huku akieleza wamejipanga vizuri katika kuhakikisha wanaenzi kampeni ya kutunza mazingira na hasa kwa kuja na mipango mbalimbali ili wananchi wengi wasitumie nishati ya kuni na mkaa ambayo kwa kiwango kikubwa inaharibu mazingira.


Akieleza zaidi Mavunde amesema anawashukuru Kampuni ya Oryx chini ya uongozi wa Araman Benoite kwa kukubali ombi lao la kuwashika mkono Baba na Mama Lishe wa Dodoma Mjini kwa kuwapatia majiko ya gesi 500 na kazi yao kubwa ni kuhakikisha wanalinda mazingira.


Pia amewashukuru kwa mafunzo yaliyotolewa na Oryx kwa Baba na Mama Lishe kuhusu matumizi sahihi ya gesi kwa ajili ya kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza huku akiwataka waliopewa kwenda kutumia majiko hayo kutunza mazingira lakini kujiimarisha kiuchumi kupitia chughuli wanazozifanya.


“Nichukue fursa hii kumshukuru Rais Dk.Samia Samia Suluhu Hassan ambaye yeye ndio muasisi wa utunzaji mazingira kwa kutumia nishati safi na alitoa maelekezo kwamba ifikapo mwaka 2032 basi asilimia 80 ya wananchi wawe wanatumia nishati safi ili kuondokana na uchafuzi wa mazingira ambao umesababisha mabadiliko ya tabianchi kwa kiwango kiwango kikubwa.


“Tunamshuku Rais Samia kwa kuweka kipaumbele na kuwa kidede kusimamia jambo hili na kama mnavyoweza kuona mitingu ambayo imetolewa hapa itapunguza matumizi ya mkaa na tukipunguza matumizi ya kuni na mkaa tututakuwa tumepunguza uharibifu wa mazingira pamoja na kulinda afya zetu kwani tunatambua watumiaji wa kuni na mkaa wamekuwa wakipata madhara ya kiafya kwa kuvuta moshi na hasa baba na mama lishe.”


Amesema kampeni ya Rais Samia kuhamasisha nishati safi inakwenda kuokoa maisha ya baba na mama lishe ambao kwa sehemu kubwa muda wao mwingi unatumika kupika na wengi wao wanatumia kuni na mkaa, hivyo kupitia nishati hiyo wanakwenda kuepukana na madhara ya kiafya yanayotokana na matumizi ya kuni na mkaa.


Awali Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini Alhaj Jabiri Shekimweri amepomngeza Waziri Mavunde kwa jinsi anavyojitoa kwa ajili ya wananchi wa Jimbo la
Dodoma Mjini wakiwemo Baba na Mama Lishe huku akitumia nafasi hiyo kusisitiza ni vema walipewa mitungi ya gesi na majiko yake kuhakikisha wanaitumia vema gesi hiyo ili wasipate madhara.


“Nitoe rai kwa wote ambao wamepatiwa gesi hii,kabla ya kuitumia wapate elimu kuhusu namna nzuri ya kutumia gesi bila kupata madhara.Nimefurahi kusikia Oryx pamoja na kutoa mitungi hii wameamua kutoa na elimu kuhusu matumizi sahihi ya mtungi wa gesi.”


Wakati huo huo Mbunge wa Viti Maalum kupitia la Asasi za Kiraia kwa tiketi ya CCM akitoa salamu kupitia Mkoa wa Kagera amesema Neema Rugangira amesema anaelewa changamoto ambazo wanawake wanazipitia katika kuandaa chakula nyumbani.


“Kunachangamoto za akina mama kutumia muda mwingi kwenda kutafuta kuni , watoto wanatumia muda mwingi kwenda kutafuta kuni.Kuna kadhia nyingi ambazo tunazipitia wakati wa kwenda kutafuta kuni ikiwemo ukatili wa kijinsia , muda mwingi tunaotumia kutafuta kuni muda ule tungeweza kufanya shughuli nyingine za kiuchumi.


“Kwahiyo Rais Dk.Samia Suluhu Hassan alipokuja na ajenda ya kutafuta nishati safi na salama ya kupikia moja ni kuokoa afya zetu kwani akina mama na watoto wanapata madhara makubwa kutokana na moshi ule ambao tunavuta wakati wa kupika,”amesema.


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages