Breaking

Monday 29 January 2024

DAWASA KUSHIRIKIANA NA TAASISI ZA KIRAIA KUTUNZA MAZINGIRA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imedhamiria kushirikiana na wadau / Taasisi za kiraia katika utunzaji wa Mazingira ili iwe jamii iweze kunufaika na mazingira yanayowazunguka.

DAWASA ni miongoni mwa wadau walisoshiriki zoezi la kupanda miti wakati wa hafla ya uzinduzi wa ofisi za taasisi inayoshughulika na Utunzaji wa Mazingira na Ufundishaji wa stadi za maisha (Acceleration of Life Skills Foundation-ALSF) iliyopo kata ya Mabwepande Jijini Dar es Salaam.

DAWASA imeahidi kuwa bega kwa bega na Taasisi hiyo katika utoaji wa elimu ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira kando ya barabara na pembezoni mwa Mto Mpiji na Mto Magoza yaliyopo ndani ya eneo la kihuduma la Mamlaka.


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages