Breaking

Friday, 8 December 2023

WiLDAF YAKABIDHI TUZO KWA VINARA 16 WA KUPAMBANA DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA 2023

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la WiLDAF, Anna Kulaya akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Tuzo kwa Vinara 16 wa Kupambana Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia kwa mwaka 2023 

Vinara 16 wa Kupambana Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia 2023.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF) ambalo linaratibu Mtandao wa Kupambana na Ukatili wa Kijinsia (MKUKI) limetunuku Tuzo kwa Vinara 16 wa Kupambana Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia zenye lengo kutambua na kupongeza juhudi za watu binafsi waliochukua hatua kubwa na za kipekee katika kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii zao na Tanzania kwa ujumla.

Tuzo kwa Mabingwa 16 Wanaopinga Ukatili wa Kijinsia zimekabidhiwa leo Alhamisi Desemba 7,2023 jijini Dar es salaam  na mabalozi wa nchi mbalimbali pamoja na Wakurugenzi wa LSF na Care Tanzania (Lulu Ng'wanakilala na Prudence Masako) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku 16 za Uanaharakati dhidi ya kupinga Ukatili wa Kijinsia 2023 yenye kauli mbiu ‘Wekeza kuzuia ukatili wa kijinsia’.

Vinara 16 wa Kupambana Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia mwaka 2023 waliopata tuzo ni Geah Habib (Dar es salaam), Valerian Felix Mgani (Mara), Zinduna Abdallah (Tabora), Mwita Nyasibira (Mara), Padre Dennis Ombeni (Arusha), Devotha Tweve (Songwe), Aluwa Mkilindi (Dar es salaam), Sophia Issa (Njombe), Mpulan Kashindye (Mara), Nassoro Haji Juma (Zanzibar), Lydia Charles (Dar es salaam), Salha Aziz (Dar es salaam), Veronica Kidemi (Arusha), Robert Mmary ‘Mzee Nyoka’ (Kilimanjaro),Eden Ezekiel Wayimba (Katavi) na Edwin Mugambila (Dar es salaam).

Pia Mwanaharakati na Mdau katika uimarishwaji wa haki za watoto wa kiume, Anna Homstrom amepatiwa Tuzo ya  heshima ya  kusimamia utetezi wa upatikanaji wa haki za binadamu hasa kupinga vitendo vya udogoshwaji wa watoto wa kike kwa kufanyiwa ukeketaji.

Awali akizungumza, Jaji Mkuu wa Shindano la Tuzo hizo, Dkt. Katanta Simwanza ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika la Miracle Corners of Tanzania amesema washindi wa tuzo hizo walipatikana kupitia mchakato wa mapendekezo ya wanajamii kwa kutoa majina ya watu wanaofanya harakati za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye jamii baada yah apo watu hao walifanyiwa usahili na kwa kila tuzo walipatikana watu watatu ambapo tuzo zipo 16 na washindi wa nafasi za kwanza ndiyo wamepatiwa tuzo.

“Tunashangilia kuwapatia tuzo hizi na kutokana na uzoefu kwa miaka minne iliyopita washindi wote wa tuzo wameendelea kufanya kazi vizuri kwenye jamii za kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia. Mathalani tunashuhudia Suleiman Bishagazi na Msafiri Mwajuma ambao wamekuwa wakifanya kazi nzuri kiasi kwamba serikali kupitia Waziri wa Maendeleo Jinsia na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima anatambua mchango wao kwenye jamii”,amesema Dkt. Simwanza.
Jaji Mkuu wa Shindano la Tuzo kwa Vinara 16 wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia, Dkt. Katanta Simwanza.

“Katika harakati za kuzuia ukatili wa kijinsia ushirikishwaji wa wanaume ni jambo la muhimu sana kama alivyoeleza ndugu Abubakar Rehani wa kutoka Mradi wa Afya Yangu _TMARC kwamba wanaume wao hushiriki moja kwa moja kutatua changamoto za wanawake, pia wanachangamoto zao za kufanyiwa ukatili wa kijinsia, afya ya akili ,magonjwa na ndiyo vinara wa kuleta mabadiliko katika jamii zetu kwani wao ndiyo watoa maamuzi kwenye ngazi za familia, watoa maamuzi, watunga sera, wamiliki rasilimali katika ngazi ya jamii”,ameongeza Dkt. Simwanza.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo hizo za Vinara 16 katika kuzuia ukatili wa kijinsia mwaka 2023, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la WiLDAF, Anna Kulaya amesema tuzo hizo zimeandaliwa na Shirika la WilDAF ikiwa ni ishara ya kuwatambua mashujaa katika mapambano ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

“Huu ni mwaka wa nne sasa WiLDAF tunaandaa Tuzo kwa Vinara 16 wa Kuzuia Ukatili wa Kijinsia, tuzo hizi tunazitoa kwa watu/watanzania wa kawaida kabisa tukiwatambua na kuwatia moyo kwa namna wanavyojituma kupinga ukatili wa kijinsia. Mwaka huu tulipokea maombi zaidi ya 700 wakiwania tuzo hizi, tunayo furaha kuona wanaume 8 na wanawake wameshinda tuzo hizi. Kwa kweli simulizi na hadithi ya kila mmoja alichokifanya zinagusa sana”,ameeleza Kulaya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la WiLDAF, Anna Kulaya.

Amesema kutokana na mwitikio mkubwa wa wanaume kuwa mstari wa mbele kupinga ukatili wa kijinsia ikiwemo kupinga mila kandamizi dhidi ya wanawake na watoto, amesema endapo wanaume wengi wataendelea kujitokeza kuzuia ukatili wa kijinsia hakika mapambano kupinga ukatili wa kijinsia yatakuwa rahisi sana na kuifanya jamii kuwa salama.

“Wanaofanya vitendo vya ukatili wengi ni wanaume, hawa ndiyo baadhi yao wanabaka na kulawiti watoto. Tunataka wanaume walinde jamii, walinde familia’,ameeleza.

Katika hatua nyingine ameitaka jamii kuvunja ukimya na kuepuka kunyamazia vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuvumilia ukatili badala yake watoa ushirikiano polisi na mahakamani huku akivishukuru vyombo vya habari kuendelea kuibua na kufichua matukio ya ukatili wa kijinsia na kuyaomba kufanya mwendelezo hadi tamati ya kesi za matukio hayo.

Akizungumza kwa niaba ya Washindi wa Tuzo hizo, Padre Dennis Ombeni wa Jimbo Katoliki Arusha amewaomba washindi wenzake kuendelea kupaza sauti dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia huku akizitaja baadhi ya changamoto zinazokwamisha kesi za matukio ya ukatili wa kijinsia kuwa ni pamoja na wananchi kutotoa ushahidi mahakamani, usiri wa jamii kufichua matukio ya ukatili.

“Wito wetu ni kuvunja ukimya kuhusu matukio ya ukatili wa kijinsia. Ukweli ni kwamba kutotoa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia ni kutengeneza bomu lijalo. Tunaomba wadau waendelea kutoa elimu na ushauri kwa jamii, kuwa wepesi wa kutoa taarifa kuhusu matukio mfano ukeketaji na wadau kushirikiana na serikali,mashirika kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia”,amesema Padre Ombeni.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la WiLDAF, Anna Kulaya akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Tuzo kwa Vinara 16 wa Kupambana Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia kwa mwaka 2023 Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la WiLDAF, Anna Kulaya akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Tuzo kwa Vinara 16 wa Kupambana Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia kwa mwaka 2023 
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la WiLDAF, Anna Kulaya akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Tuzo kwa Vinara 16 wa Kupambana Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia kwa mwaka 2023 
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la WiLDAF, Anna Kulaya akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Tuzo kwa Vinara 16 wa Kupambana Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia kwa mwaka 2023 
Jaji Mkuu wa Shindano la Tuzo kwa Vinara 16 wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia, Dkt. Katanta Simwanza ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika la Miracle Corners of Tanzania akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Tuzo kwa Vinara 16 wa Kupambana Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia kwa mwaka 2023 
Mwakilishi wa Washindi wa Tuzo, Padre Dennis Ombeni akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Tuzo kwa Vinara 16 wa Kupambana Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia kwa mwaka 2023 
Mwanaharakati na Mdau katika uimarishwaji wa haki za watoto wa kiume, Anna Holstrom akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Tuzo kwa Vinara 16 wa Kupambana Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia
Mwakilishi wa Jeshi la Polisi akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Tuzo kwa Vinara 16 wa Kupambana Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia
 Mmoja wa washindi wa Tuzo ya Vinara 16 wa Kupambana Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia, Geah Habib kutoka Dar es salaam (kulia) akipokea tuzo

Mmoja wa washindi wa Tuzo ya Vinara 16 wa Kupambana Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia, Valerian Felix Mgani kutoka mkoani Mara (kulia) akipokea tuzo
Mmoja wa washindi wa Tuzo ya Vinara 16 wa Kupambana Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia, Zinduna Abdallah kutoka mkoani Tabora (kulia) akipokea tuzo

Mmoja wa washindi wa Tuzo ya Vinara 16 wa Kupambana Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia, Mwita Nyasibira kutoka mkoani Mara (kulia) akipokea tuzo

Mmoja wa washindi wa Tuzo ya Vinara 16 wa Kupambana Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia, Padre Dennis Ombeni kutoka mkoani Arusha (kulia) akipokea tuzo
Mmoja wa washindi wa Tuzo ya Vinara 16 wa Kupambana Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia, Devotha Tweve kutoka mkoani Songwe (kulia) akipokea tuzo
Mmoja wa washindi wa Tuzo ya Vinara 16 wa Kupambana Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia, Aluwa Mkilindi kutoka Dar es salaam (kulia) akipokea tuzo

Mmoja wa washindi wa Tuzo ya Vinara 16 wa Kupambana Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia, Sophia Issa kutoka mkoani Njombe (kulia) akipokea tuzo
Mmoja wa washindi wa Tuzo ya Vinara 16 wa Kupambana Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia, Mpulan Kashindye kutoka mkoani Mara (kulia) akipokea tuzo
Mmoja wa washindi wa Tuzo ya Vinara 16 wa Kupambana Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia, Nassoro Haji Juma kutoka Zanzibar (kulia) akipokea tuzo
Mmoja wa washindi wa Tuzo ya Vinara 16 wa Kupambana Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia, Lydia Charles kutoka Dar es salaam (kulia) akipokea tuzo
Mwakilishi wa Mshindi wa Tuzo ya Vinara 16 wa Kupambana Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia, Salha Aziz (kulia) kutoka Dar es salaam akipokea tuzo
Mmoja wa washindi wa Tuzo ya Vinara 16 wa Kupambana Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia, Veronica Kidemi kutoka mkoani Arusha (kulia) akipokea tuzo
Mmoja wa washindi wa Tuzo ya Vinara 16 wa Kupambana Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia, Robert Mmary  kutoka mkoani Kilimanjaro (kulia) akipokea tuzo
Mmoja wa washindi wa Tuzo ya Vinara 16 wa Kupambana Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia, Eden Ezekiel Wayimba kutoka mkoani Katavi (kulia) akipokea tuzo
Mmoja wa washindi wa Tuzo ya Vinara 16 wa Kupambana Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia, Edwin Mugambila kutoka Dar es salaam (kulia) akipokea tuzo
Mwanaharakati na Mdau katika uimarishwaji wa haki za watoto wa kiume, Anna Holstrom (kulia) akipokea Tuzo maalum ya kusimamia utetezi wa upatikanaji wa haki za binadamu hasa kupinga vitendo vya udogoshwaji wa watoto wa kike kwa kufanyiwa ukeketaji.
Wadau wakifuatilia matukio wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa Vinara 16 wa Kupambana Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia 2023
Burudani ikiendelea wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa Vinara 16 wa Kupambana Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia 2023

Vinara wa Kupambana Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia 2023 wakionesha tuzo zao

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages