Breaking

Thursday 7 December 2023

WAZIRI SILAA AKAGUA ENEO MBADALA LA WAHANGA MAFURIKO HANANG



Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa amekagua eneo mbadala watakapohamishiwa wahanga wa mafuriko yaliyotokea katika mji mdogo wa Kateshi wilaya ya Hanang mkoani Manyara manamo tarehe 3 Desemba 2023.

Waziri Silaa ameongozwa na Kaimu Afisa Ardhi wa wilaya ya Hanang Erick Mbeya ambaye amemuonesha eneo lililopo kata ya Jorodom Kitongoji cha Gwadaat eneo la mji mdogo wa Kateshi wilaya ya Hanang.

Eneo hilo lina takriban ekari 216.01 ambapo viwanja 450 vinapimwa na mashamba 50 ya kilimo cha mjini yatatengwa kwa ajili ya wahanga hao.

Aidha, eneo hilo kwa sasa linamilikiwa na wananchi wa asili ambapo utaratibu wa utwaaji unafanyika kwa mujibu wa sheria.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages