Breaking

Wednesday, 20 December 2023

TGNP, VITUO VYA TAARIFA NA MAARIFA KUUNGANA NA ASASI ZA KIRAIA KUPAMBANIA MAMBO YENYE MLENGO WA KIJINSIA

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) imeendaa warsha ya Mafunzo kwa ajili ya kuwaongezea ujuzi wanaharakati wa Jinsia kutoka Vituo vya Taarifa na Maarifa pamoja na wadau kutoka Asasi za kiraia,kwa lengo la kuwaunganisha Wanaharakati hao na Asasi za kiraia ambapo Utaundwa mpango kazi ambao utashirikisha pande zote kufanya kazi kwa pamoja.

Hayo yamesemwa Dec 20,2023 Mabibo, Jijini Dar es Salaam katika ofisi za TGNP na Mratibu wa Mafunzo kutoka TGNP, Bi. Anna Sangai amesema wanaamini vituo vya taarifa na maarifa vinafanya juhudi kubwa ili kuleta mabadiriko katika jamii.

"Ili kuongeza hiyo juhudi tumewaunganisha na Asasi za kiraia ambazo zipo katika mikoa ili waweze kuandaa mpango kazi kuweza kufanya kazi kwa pamoja na tunaamini ujenzi wa nguvu za pamoja utapatikana". Amesema Sangai.

Aidha Bi.Sangai ameeleza kwamba wamewakutanisha kwa lengo la kuelezea na kutathimini kazi ya vituo vya taarifa na maarifa kwa mwaka mzima na kubainisha maeneo ya ushirikiano katika mpango kazi wa mwaka 2024.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kituo Cha Taarifa na Maarifa Cha Zirai kilichopo mkoani Tanga, Bi.Joyce Mdoe amesema kuwa baada ya kupewa mafunzo kutoka mtandao wa Jinsia nchini wameweza kupata wakunga wanawake katika Zahanati yao ambapo awali mama wajawazito walipata changamoto ya kuzalishwa na wakunga wakiume hali iliyopelekea kuona aibu na kusababisha wengi kujifungulia nyumbani.

"Sasa hivi tunamafanikio makubwa kwamba kwenye Zahanati yetu Kuna wakunga wawili wa kike Tena wenye umri mkubwa kwahiyo mama mjazito anyae enda kuzalishwa pale haogopi kitu chochote anazalishwa tu". Amesema Bi. Joyce.

Bi. Joyce ametoa wito kwa Mtandao wa Jinsia TGNP kuendelea kutoa elimu katika maeneo yao kwenye uongozi wa ngazi za chini kwasababu hata wanaposema jambo hawaelewi kwa sababu hawakuhudhuria mafunzo ya awali.

Naye Katibu kutoka Kituo Cha Taarifa na Maarifa kutoka Kata ya Shilela,halmashauri ya Msalala,Wilaya ya Kahama Bw.Joseph Samweli amesema baada ya kupata mafunzo kwa wadau wa masuala ya Jinsia kwenye vituo taarifa na maarifa maendeleo yameanza kuonekana hasa kwenye upande wa miundombinu mbalimbali.

Warsha hiyo itahusisha wadau wa Jinsia kutoka vituo vya taarifa na maarifa pamoja na Asasi za kiraia kutoka mikoa ya Kilimanjaro,kigoma,morogoro, Shinyanga,Mara,Mtwara na Tanga.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages