NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limewataka wamiliki wa maeneo ya uchimbaji na uchenjuaji wa madini hususani kwenye mabwawa ya majitaka, topesumu na maeneo ya kutunzia miamba ya sumu kuhakikisha maeneo hayo hayaleti madhara kwa jamii na vyanzo vya maji kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.
Wito huo umetolewa leo Desemba 11,2023 Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Bw. Menan Jangu wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za NEMC.
Amesema taarifa kutoka katika Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) zinaonesha kuwa mvua za viwango tofauti zitaendelea katika maeneo mbalimbali nchini ambapo mvua hizo zimekuwa kubwa na kuendelea kusababisha madhara kadhaa wa kadhaa.
Aidha amesema wananchi wanatakiwa kuepuka kukaa katika maeneo ya fukwe za bahari ikiwa ni pamoja na kandokando ya maziwa na mito na wanaoishi kwenye milima na maeneo ya kandokando wanatakiwa kuchukua tahadhari mapema.
Amesema kuwa wananchi wanatakiwa kuwa na umakini na matumizi ya maji majumbani na kuhakikisha tahadhari zinachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuchemsha maji ya kunywa pia wanakumbushwa kutokutiririsha majitaka kwenye mifereji ya maji ya mvua.
"Wananchi wanakumbushwa kuzingatia Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004, Kifungu No. 57 na kuepuka ujenzi kwenye maeneo hatarishi ikiwa ni pamoja na maeneo ya kando ya mito, fukwe za bahari na maeneo ya ardhi oevu". Amesema
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Bw. Menan Jangu akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 11,2023 katika Ofisi za NEMC Jijini Dar es Salaam