Fundi Sanifu wa Ujenzi kutoka Kampuni ya EEG LTD Bw. Steven Malima (wa kwanza kushoto) akitoa taarifa ya ujenzi wa ofisi mpya ambayo imejengwa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma kwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Mcha Hassan Mcha (wa tatu kulia) wakati alipotembelea wilayani humo kwa ajili ya kuona maendeleo ya ujenzi wa ofisi hiyo.
Mshauri wa Ujenzi Bw. Berson Kayanda (wa pili kulia) akizungumza na Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Mcha Hassan Mcha (wa pili kushoto) wakati alipotembelea Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma kwa ajili ya kuona maendeleo ya ujenzi wa ofisi mpya ya TRA inayojengwa wilayani humo.
Ofisi mpya ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA inayojengwa katika Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma ikiwa hatua za mwisho za ujenzi.
Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Mcha Hassan Mcha (katikati) akizungumza na watumishi wa TRA Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wakati alipotembelea wilaya hiyo kwa ajili ya kuona maendeleo ya ujenzi wa ofisi mpya ya TRA inayojengwa wilayani humo.
Afisa Msimamizi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma Bw. Baraka Laiza akitoa maoni yake kwa Naibu Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Mcha Hassan Mcha wakati Naibu Kamishna Mkuu huyo alipotembelea wilaya hiyo kwa ajili ya kuona maendeleo ya ujenzi wa ofisi mpya ya TRA inayojengwa wilayani humo.
Afisa Msimamizi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma Bw. Musa Joseph akitoa maoni yake kwa Naibu Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Mcha Hassan Mcha (hayupo pichani) wakati Naibu Kamishna Mkuu huyo alipotembelea wilaya hiyo kwa ajili ya kuona maendeleo ya ujenzi wa ofisi mpya ya TRA inayojengwa wilayani humo.
Baadhi ya Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Kigoma wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Mcha Hassan Mcha (katikati) wakati Naibu Kamishna Mkuu huyo alipotembelea Wilaya ya Kasulu kwa ajili ya kuona maendeleo ya ujenzi wa ofisi mpya ya TRA inayojengwa wilayani humo. (Picha zote na TRA)