Rais wa wanazuoni wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Prof. Modest Diamond Varisanga, anayoheshima kubwa kuwaalika wanazuoni wote wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, wajumbe wa Baraza la Chuo na Seneti, wananchi na wadau wote wa elimu nchini kuhudhuria mkutano wa 33 utakaofanyika Disemba 13, 2023 katika ukumbi wa kituo cha Chuo Kikuu Huria cha Tanzania mkoa wa Ruvuma mjini Songea kuanzia Saa Mbili kamili Asubuhi.
Mada kuu katika mkutano huo ni "Matokeo ya marejeo ya Sera mpya ya Elimu ya mwaka 2023 na matarajio ya Taasisi za Elimu ya juu nchini."
Mada hii itawasilishwa na mzungumzaji mkuu Prof. Makenya Maboko na kujadiliwa na wanamjadala Prof. Elifas Bisanda na Prof. Deus Ngaruko na kisha kujadiliwa na washiriki wote.
Mkutano huu utarushwa mubashara kupitia vyombo mbalimbali vya mitandao ya kijamii.
Mkutano huu utafuatiwa na Mahafali ya 42 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yatakayofanyika Disemba 14, 2023 kuanzia Saa Mbili kamili Asubuhi kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Nyote Mnakaribishwa
Imetolewa na:
Dkt. Mohamed Omary Maguo
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
Songea
11/12/2023