Imebainishwa kuwa elimu duni ya matumizi ya mikopo kwa watanzania imeonekana kuwa mwiba kwao kwani wengi wao wamekua wakikopa kwa shughuli nyingine nje ya biashara hali ambayo imekemewa na taasisi za kifedha nchini.
Akizungumza Jijini Dar es salaam katika uzinduzi wa jengo jipya la tawi na makao makuu ya benki ya Mkombozi Baba Askofu Mkuu wa jimbo la Dar es salaam Jude Ruwai’chi amesema miongoni mwa mikopo inayofifisha maendeleo ni pamoja na kausha damu.
Amesema watanzania wanapaswa kuomba mikopo katika taasisi za kibenki pamoja na kuheshimu dhamira ya mikopo hiyo huku akitumia nafasi hiyo kuwashahuri wanaokopa kujikita katika biashara.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji benki ya Mkombozi, Respite Kimati amesema tayari benki hiyo imeanza kutumia nyenzo za teknolojia katika kufikisha huduma za kibenki kwa watanzania hasa maeneo ya vijijini.
Uzinduzi wa jengo wa hilo umehudhuriwa na viongozi wa mbalimbali ikiwemo wajumbe wa bodi huku mkakati uliopo kwa mwaka ujao ni kupanua wigo wa huduma hizo kwa kuongeza matawi mengi zaidi.