Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imekusudia kubadilisha miundombinu chakavu ya Majisafi katika eneo lake la kihuduma katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kwa umbali wa kilomita takribani 400 kwa mwaka wa fedha 2023/2024
Maboresho hayo yanalenga kuimarisha huduma na kudhibiti kiwango cha maji kinachopotea kutoka asilimia 37 hadi asilimia 20.
Hayo yamebainishwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Ndugu Kiula Kingu katika mahojiano na vyombo vya habari hivi karibuni.
"Miundombinu ya maji katika jiji la Dar es Salaam ni ya muda mrefu kuanzia mwaka 1970 na kuendelea, mengi ni ya chuma na yameshapoteza uwezo wa kuhimili kiwango cha maji kinachozalishwa sasa tofauti na miaka ya nyuma hivyo kupeleke uvujaji mkubwa wa maji katika maeneo mengi tunayohudumia." alisema Kingu
Ametoa wito kwa Wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa DAWASA kwa kutoa taarifa bila kuchoka wakati Mamlaka ikiendelea na jitihada za kubadilisha mtandao ya majisafi ambao kwa sasa ni zaidi ya kilomita 7000.
"Tumeweka nguvu kubwa katika mapinduzi ya Teknolojia ili kugundua upotevu unapotokea kwa utaalamu wa kisayansi zaidi huku tukiendelea kutumia mafundi kwa haraka zaidi na kufanyia kazi" alisema Kingu.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990