Breaking

Friday 24 November 2023

ZINGA HADI BAGAMOYO WAITWA MAUNGANISHO MAPYA YA MAJI

Wakazi wa maeneo ya Zinga, Kiromo, Yombo, Nianjema, Magomeni, Kisutu na Dunda katika Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani waliokamilisha taratibu za kupata huduma ya Maji wametakiwa kujitokeza katika ofisi ya DAWASA BAGAMOYO ambapo zoezi la utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya inaendelea.

Zoezi hilo linaenda sambamba na utoaji elimu ya utunzaji wa miundombinu ya maji, matumizi sahihi ya maji, njia rasmi za mawasiliano za DAWASA, malipo ya ankara na huduma nyingine zitolewazo na DAWASA.

Wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja namba 0800110064 (Bure) au 0738 096 082 (DAWASA Bagamoyo).




Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages