Breaking

Wednesday, 29 November 2023

WANASAYANSI WATAKIWA KUFIKISHA TAARIFA ZA UTAFITI KWA JAMII ILI ZIWAFIKIE WALENGWA.

Naibu katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Maghembe amewataka wana sayansi nchini na wadau wa afya kufanya tafiti zitakazosaidia kuleta suluhisho juu ya changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya afya hasa changamoto kubwa ya unyanyapaa katika jamii jambo linalochangia kwa kiasi kikubwa kuzorotesha juhudi za serikali na wadau wa maendeleo katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt.Grace Maghembe wakati akifunga Kongamano la Kitaifa la Kisayansi lililofanyika katika Hoteli ya Nashera Mkoani Morogoro ambapo wadau na wataalamu wa masuala ya sayansi na tafiti walikutana kwa siku mbili kujadiliana kwa pamoja juu ya tafiti mbalimbali walizofanya zenye lengo la kutoa mwelekeo dhidi ya Maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI.

‘’Serikali itaendelea kujivunia wanataaluma wetu hasa wanaofanya tafiti za ndani zitakazoleta suluhisho katika jamii hasa kwenye sekta ya afya,na hakikisheni hizo tafiti mnazofanya ziwekwe kwenye lugha rahisi ambayo kila mtanzania ataelewa nini kimeandikwa na mzisambaze hadi ngazi ya chini kabisa ya serikali za Mitaa ilikusudi kila mtanzania aweze kunufaika na hayo machapisho yenu ya kitaalamu’’.AlisemaDkt Grace Maghembe Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya.

Aidha aliipongeza TACAIDS kwa uratibu wa kongamano hilo lililokutanisha wataalam na kujadili masuala muhimu yenye lengo la kutatua changamoto katika sekta ya afya hasa namna ya kujikinga na maambukizi mapya ya VVU na UKIMWI,alipongeza pia uwepo wa kongamano la vijana na wadau kusaidia uwezeshaji wa makongamano hayo yenye tija kubwa kwa vijana pia ni sehemu muhimu ya kupata maoni yao ili kujua ni namna gani serikali inaweza kuwekeza katika afua zinazowalenga. Hivyo kwa kufanya kungamano la vijana wa vyuo vikuu na hili lililofanyika hapa hoteli ya Nashera kwa siku mbili ambalo limekutanisha wataalamu na wadau mbalimbali wa masuala ya kisayansi katika kujadiliana kwa pamoja juu ya tafiti zilizofanywa zinatoa taswira gani kama taifa kwenye mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI.

Dkt Grace Maghembe amesema kongamano hili lilikuwa na lengo la kukaa kwa pamoja kwa wadau na kujitathimini tunafanya kazi serikali pamoja na wadau wamaendeleo kutekeleza afua mbalimbali lakini pia na kufanya tafiti kwa wakati ilikuona namna ya kutekeleza afua mbalimbali katika kudhibiti maambukizi ya virusivya UKIMWI.

Amongeza kuwa, kupitia kongamano hili litasaidia serikali kuona kazi zilizofanyika mambo gani yaliyofanyika vizuri na mambo gani ambayo haya kufanyika vizuri na kutuonyesha mambo gani ya kujifunza kutoka taasisi mbalimbali,Aidha kupitia majadiliano haya yatatuwezesha kuandaa sera itakayotekelezwa kwa jamii kwasababu tayari tumeshafahamu nini jamii inahitaji huko ngazi za chini na kwakuwa tayari tumeshapata taarifa za kitaalamu za kitafiti.

Aidha ameongeza kwa kusema kuwa lazima tupambane kuhakikisha ili kufikia malengo ya 20/30 lazimatuangalietumefikiawapikwenyejitihadazamapambanokuanzialeolakini pia kuna changamoto kubwa kuhusiana na changamoto ya kukabiliana maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto lazima iende kwa vitendo na amesema tumepiga hatua kubwa kwenye unyanyapaa lakini bado kuna changamoto kubwa ya unyanyapaa hadi leo watu wanaogopa kujitokeza kujitangaza kuwa anamaambukizi wa na kuwa hawako huru kuzungumza kwa familia na marafiki na waathirika wanavyokaa kimya ndio kunasababisha kuongezeka kwa maambukizi mapya jambo ambalo linahitaji tafiti za kina kuhusu suluhisho la kupambana na unyanyapaa katika Jamii.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages