MKUU wa Tawi la Utumishi Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Meja Jenerali Marco Elisha Gaguti amewavisha nishani kikosi cha Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania (TANBAT6) wanaolinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Akitoa taarifa kwa umma akiwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ofisa Habari wa kikosi hiyo, Kapteni Mwijage Inyoma amesema Meja Jenerali Gaguti amewapongeza askari wa kikosi hicho kwa kuvishwa nishani hiyo ya Ulinzi wa Umoja wa Mataifa.
Aidha Kapteni Inyoma amesema katika hotuba yake Meja Jenerali Gaguti alifikisha pia salaam za Mkuu wa Majeshi ya JWTZ, Jenerali Jacobo Mkunda na kutoa pongezi kubwa kwa kazi nzuri znazofanywa na kikosi hicho.
"Kikosi kinafanya kazi nzuri na kuiwakilisha nchi vema ndani ya Umoja wa Mataifa (UN) katika ulinzi wa amani ndani y Afrika ya kati ikiwa ni pamoja na kutimiza wajibu wao kama wanajeshi na kudhilisha kutimiza lengo la Umoja wa Mataifa na kutunukiwa nishani," amesema
Aidha amesema kikosi cha TANZBAT6 walianza jukumu la ulinzi wa amani Desemba 2022 na wametekeleza vema jukumu la kulinda raia ,na kukabiliana na migogoro inaendelea nchini Jamhuri ya Afrika ya kati Kwa kufanya doria za masafa marefu na mafupi ikiwa ni lengo la kudhibiti ualifu unaofanyanwa na waasi wanaovuruga nchi hiyo.