Breaking

Tuesday, 7 November 2023

WAKUU WA IDARA NA VITENGO MANISPAA YA TABORA WAPOKEA SALAMU ZA MHE.MCHENGERWA

Tabora-MC,

Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora Ndugu Elias M. Kayandabila amewasilisha maelekezo na wito mahsusi wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe.Mohamedi Mchengerwa kwa Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora leo Novemba 6,2023 katika kikao cha kawaida cha Morning Session katika ukumbi wa Manispaa ya Tabora.

Ndugu Kayandabila amewataka Wakuu wa Idara na Vitengo kusikiliza kwa makini video ya Mhe.Waziri akiwa Bungeni Novemba 4,2023 akichangia hoja za taarifa za kamati za kudumu za Bunge kuhusu Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ( CAG).

Novemba 4,2023 ,Mhe.Mchengelwa akiwa Bungeni alieleza kuwa kwa sasa lugha ni moja tu ya kufanya kazi. Alifafanua kuwa hatowafumbia macho wafanyakazi wazembe na wabadhilifu wa fedha za Umma na huku akitolea mfano wa Wakurugenzi na Wakuu wa Idara ambao ameshawachukulia hatua za kinidhamu na akasisitiza kuwa ataendelea kuchukua hatua mara moja kwa mtumishi yeyote mzembe na mbadhilifu aliepo chini ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora amewataka Wakuu wa Idara na Vitengo wa Manispaa ya Tabora kujitafakari kwa kina kama wao wanafanya kazi kwa kiwango gani na ni wabadhilifu ama si wabadhilifu wa fedha za Serikali kwa kiwango gani, aidha akawasisitiza Wakuu wa Idara kuwa waache kufanya kazi kwa mazoea, waende na kasi ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha Ndugu Kayandabila ametanabaisha kuwa, hatosita kumchukulia hatua Mkuu wa Idara ama Kitengo mzembe ama mbadhilifu wa fedha za Serikali kwa nafasi yake kama Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora, hivyo amewataka Viongozi hawa walio chini yake waongeze tija, morali na ufanisi katika kazi zao kwa kuzingatia weredi wa taaluma zao.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages