NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
WADAU wa semina za Jinsia na maendeleo (GDSS) wameendelea kujivunia Tamasha la 15 lililofanyika Novemba 7-10 katika Viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Mabibo Jijini Dar es Salaam ambapo wameelezea faida za ushiriki wa Tamasha hilo ambalo lilikuwa la kuvutia kwa wageni pamoja na wenyeji washiriki.
Akizungumza leo Novemba 22, 2023 Jijini Dar es Salaam, Mdau wa masuala ya Jinsia na Maendeleo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kituo Cha Taarifa na Maarifa Kata ya Majohe, Bi.Tabu Ally amesema kuwa Tamasha hilo limekuwa na umuhimu mkubwa hasa kwa wanawake kwani inawapatia fursa ya kujijenga zaidi na kuwapa ujasiri wa kujiamini katika kila Jambo hivyo kuwapatia uwezo wao kuthubutu kufanya mambo mbalimbali.
"Kitu Cha kwanza nilicho kipata ni Umoja na kufahamiana, kitu nilichojifunza kikubwa sana ni kwenye warsha nimeamini kwamba warsha zinaweza kukujenga wewe kama mwanamke nakuweza kujiamini kwa kila kitu hicho nikitu ambacho niliona Cha muhimu sana". Amesema
Bw.Mteganda Hussein ambaye ni Mdau wa Semina za Jinsia na maendeleo (GDSS), amesema kuwa Tamasha hilo lilimpa fursa ya kutanua wigo na kujenga mahusiano na watu mbalimbali kutoka katika taasisi nyingine na ameweza kupata ujuzi juu ya umuhimu wa kufatilia afya yake ya akili.
"Kwenye Tamasha hili nilipata fursa kuhudhuria katika warsha za afya ya akili nimegundua watu wote tunatakiwa kuhudhuria katika kliniki za afya ya akili kama ilivyo kwenye magonjwa mengine nahisi ndilo jambo la msingi kwangu kwasababu kwenye jamii yetu ni vitu ambavyo havipo". Ameeleza Bw.Mteganda.
Aidha Bw.Joseph Bulemo amesema kuwa kupitia tamasha lililofanyika amejifunza nakuona manufaa kuhusu hamasa na harakati zilizo anyika katika kupambania haki na usawa wa kijinsia ambazo zimezaa matunda kwa kuwapatia haki hasa wanawake kwenye mambo ambayo hayakutiliwa mkazo zamani na kuendeshwa na mfumo dume.
Tamasha hilo lilihudhuriwa na watu zaidi ya 2000 kutoka mashirika mbalimbali nchini pamoja na nje ya nchi ambapo nchi takribani 14 ziliweza kushiriki huku mgeni Rasmi akiwa ni Makamu wa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini ambaye pia aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Shirika la UN Women Ulimwenguni Mhe. Phumuzile Mrambo.