Kaimu
Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. William Mwegoha (kulia), akisalimiana na Mkuu wa
Wilaya ya Mbarali, Kanali Dennis Mwila (kushoto), ambaye alimwakilisha Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya katika Kongamano la Miaka 20 ya Kumbukizi ya Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere.
Mkuu wa
Wilaya ya Mbarali, Kanali Dennis Mwila (Kulia), Mgeni Rasmi wa Kongamano la
Miaka 20 ya Kumbukizi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, akisalimiana na Mkurugenzi
wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere na Mzungumzaji Mkuu wa Kongamano, Mzee Joseph
Butiku (kushoto).
Mkuu
wa Wilaya ya Mbarali, Kanali Dennis Mwila, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya
katika ufunguzi wa Kongamano la Miaka 20 ya Kumbukizi ya Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere lililofanyika jijini Mbeya na kuratibiwa na Chuo Kikuu
Mzumbe.
Mkuu
wa Wilaya ya Mbarali, Kanali Dennis Mwila (katikati), Mwakilishi Wa Mgeni
Rasimi wa Kongamano la Miaka 20 ya Kumbukizi ya Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere, akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Chuo Kikuu Mzumbe, Mwendeshaji
Mkuu wa Kongamano Dkt. Ayoub Rioba na Mtoa mada Mkuu wa kongamano hilo Mzee
Joseph Butiku
Mkurugenzi
Mkuu wa TBC, na Mwongozaji Mkuu Wa Kongamano la 20 la Kumbukizi ya Hayati
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Dkt. Ayoub Rioba, akizungumza wakati wa kongamano
hilo.
Mhadhiri
kutoka Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala wa Umma, Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, Dkt. Richard Mbunda, akitoa mada juu Mtazamo wa Mwalimu Nyerere kuhusu Ulinganifu
wa Usimamizi wa rasilimali na mabadiliko ya serikali za Tanzania.
Mhadhiri
wa Sheria Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Mbeya, Dkt. Tasco Romanus Luambano, akitoa
mada juu Mtazamo wa Mwalimu Nyerere kuhusu rasilimali madini na utawala bora.
Mhadhiri
Mwandamizi wa Taasisi ya Taaluma za Maendeleo, Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Lulu
Elizabeth Genda, akitoa mada juu Mtazamo wa Mwalimu Nyerere kuhusu Jukumu la
wanawake katika kulinda rasilimali za Taifa.
Mhadhiri
Mwandamizi wa Taasisi ya Taaluma za Maendeleo, Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Theobald
Frank Theodory, akitoa mada juu Mtazamo wa Mwalimu Nyerere kuhusu makadirio na
mwelekeo wa maendeleo ya viwanda nchini tanzania.
Wanafunzi
na washiriki mbalimbali wakiuliza maswali na kuchangia mada wakati wa kongamano
la 20 la Kumbukizi ya Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere lililofanyika
Mbeya hivi karibuni na kuratibiwa na Chuo Kikuu Mzumbe.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe - Mipango, Fedha Na Utawala, Prof. Allen Mushi, akitoa neno la shukrani wakati wa kuhitimisha Kongamano la 20 la Kumbukizi Ya Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere lililofanyika Jijini Mbeya hivi karibuni