Timu za soka na Netiboli za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania- TPA zimeanza vyema kampeni ya kuwania ubingwa wa Mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi (SHIMUTA) yaliyoanza kutimua vumbi tarehe 12 Novemba 2023, Mkoani Dodoma.
Timu ya soka ya TPA imepata ushindi wa bao 1 kwa 0 dhidi ya Timu ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro- NCAA, bao hilo pekee la ushindi limetiwa kimiani na Ramadhani Madebe Katika dakika ya 15 ya mchezo.