Breaking

Thursday, 9 November 2023

TBS KUTUNUKU TUZO ZA UBORA WA BIDHAA NA HUDUMA MAADHIMISHO SIKU YA UBORA

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Kuelekea kilele cha wiki ya Ubora,Shirika la Viwango Tanzania(TBS) limeandaa maadhimisho  ya siku ya Ubora yenye lengo la kushukuru mchango wa wataalamu wa ubora katika sekta mbalimbali zinazotoa huduma na bidhaa pamoja na kupeana uzoefu ili kuendeleza kukuza Ubora na kulinda afya ya mlaji.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Nov 9,2023 Meneja Ithibati Ubora wa Bidhaa, Bi. Amina Yassin amesema kuwa ili kuwa  na uwezo katika soko la ushindani lazima kufanya tathimini na kutambua kama kuna uwezo  kufanya kitu kuwa bora na kujenga mahusiano mema na wafanyakazi.

“Kwa wazalishaji na wafanyabiashara na wadau wote wanao toa huduma na bidhaa wahakikishe wanatumia nyenzo, wanatumia kanuni za ubora ili waweze kufata zile zitasaidia kupunguza yale mapungufu ambayo binadamu anakuwa nayo wakati anafanyakazi zake na kuhakikisha ubora tunaouhitaji pia tutengeneze utamaduni wa ubora na tutambue nini wateja wetu wanataka" Amesema Bi. Amina

Aidha Bi. Amina amesema kuwa ili wazalishaji kuwa na bidhaa bora lazima kuzingatia  kanuni nne  katika usimamizi ubora maeneo ya kazi ambazo zitasaidia kuwa na bidhaa bora kwa wazalishaji hata zinapokua sokoni na kumfikia mlaji.

"Lazima tuanze kwa kuweka mipango ,mipango lazima izingatie ubora katika mipango pia tuna angalia vihatarishi na katika  hatua ya kubuni lazima tufikirie hiki kitu kinaweza kuwa bora?lazima tuweke udhibiti ambao utahakikisha bidhaa itakuwa bora, kuweka uhakika kwamba bidhaa  au huduma ikienda kwa mlaji itakuwa bora,tuboreshe sehemu yenye mapungufu ili kuendelea kuwa na bidhaa bora". Amesema.

Kwa upande wake Afisa Mkaguzi wa TBS Baraka Mbajije amesema kuwa Tanzania kama moja ya nchi ambazo zimeridhia mkataba wa Shirika la kibiashara Duniani (WTO) kumekuwa na muingiliano wa bidhaa na huduma mbalimbali hivyo lazima wazalishaji na watoa huduma watoe bidhaa na huduma ambazo zinaweza kushindana katika soko la kimataifa.

 "Tutakuwa na mijadala siku  hii katika ukumbi mpya wa maktaba ya chuo Kikuu Cha UDSM ambayo itakuwa imegawanyika katika makundi matatu,kundi la kwanza litawakutanisha wataalamu ambao Wana shughulika kwa namna moja au nyingine kwenye sekta mbalimbali katika huduma hasa usimamizi wa rasilimali watu kwenye sekta hiyo ya huduma tutajadili mafanikio changamoto na namna tunaweza kushindana ili tuweze kushindana duniani. Eneo jingine ni mamlaka ya udhibiti namna mamlaka zinavyochangia kuboresha uwepo wa bidhaa bora na huduma eneo jingine litawahusisha wazalishaji ambao wamefanikiwa kufanya biashara nje ya nchi au ndani ya nchi kwasababu wameingiza nyenzo ya Ubora ili kufikia masoko". Ameeleza Baraka
 
Pamoja na hayo amesema kuwa Tanzania ni moja ya nchi ambayo imeridhia soko huru la Afrika Jambo ambalo litafungua mipaka ya nchi na bidhaa mbalimbali zitaingia nchini ili kushindana katika soko lazima bidhaa zetu ziweze kushindana kwa kuwa na ubora.

Sambamba na hayo ameongezea kuwa kutakuwa na utoaji wa tuzo  kwa watu mbalimbali na makampuni ambayo  yamefanya vizuri kwenye maeneo mbalimbali kwenye masuala ya Ubora.

"Kundi la kwanza ni kampuni Bora ya mwaka na kundi la pili ni bidhaa bora ya mwaka,na kundi la tatu ni la watoa huduma Bora wa mwaka,na kundi la nne ni  kundi la msafirishaji Bora nje ya nchi,na kundi la tano ni kwa mtu mmoja aliyefanya vizuri aliyetoa mchango kwa kuboresha,kuimarisha au kuanzisha miundombinu ya ubora, kutakua na tuzo mbili kwa kampuni kubwa na kwa mjasiriamali mdogo"Amesema

Maadhimisho ya kilele wiki  cha Ubora  yalizinduliwa Nov 6 na kilele chake ni Nov 10,2023 yamebeba kauli mbiu isemayo UBORA TAMBUA UWEZO WAKO WAKUSHINDANA ambayo yataambana na mijadala yenye lengo la kutambua mafanikio changamoto na mbinu za kuinua Ubora.

Meneja Ithibati Ubora wa Bidhaa, Bi. Amina Yassin  (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 9,2023 katika Ofisi za Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Jijini Dar es Salaam.
Meneja Ithibati Ubora wa Bidhaa, Bi. Amina Yassin akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Novemba 9,2023 katika Ofisi za Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Jijini Dar es Salaam.
Afisa Mkaguzi wa TBS Baraka Mbajije akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Novemba 9,2023 katika Ofisi za Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Jijini Dar es Salaam.
Afisa Mkaguzi wa TBS Baraka Mbajije (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Novemba 9,2023 katika Ofisi za Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Jijini Dar es Salaam.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages