Breaking

Thursday, 16 November 2023

SERIKALI KUPITIA MKUMBI YAFUTA TOZO, KERO 231

Na. Mwandishi Wetu

SERIKALI kupitia Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara (MKUMBI) imefuta na kupunguza jumla ya tozo, ada na faini zisizopungua 232 kati ya 380 zilizobainishwa katika utekelezaji wake sawa na asilimia 61.

Akizungumza wakati wa Kikao Maalum cha Kikundi Kazi cha Mazingira ya Biashara Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amesema dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuifungua Tanzania na kuwa kivutio cha kufanya biashara na uwekezaji inatekelezeka kwa vitendo kwa ufutwaji wa tozo, ada na faini ambazo zilikuwa kero kubwa kwa ustawi, ukuaji na maendeleo ya biashara na uwekezaji hapa nchini.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi akizungumza  wakati wa Kikao Maalum cha Kikundi Kazi cha Mazingira ya Biashara Jijini Dar es Salaam, Dkt. Yonazi pia ni Mwenyekiti wa Kikosi kazi hicho. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa  la Biashara (TNBC), Dkt. Godwill Wanga na Kushoto ni Mwenyekiti Mwenza wa Kikundi Kazi hicho cha Mazingira ya Biashara, Bw. Vicent Minja
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages