Mkuu wa idara ya jinsia vijana na watu wenye ulemavu kutoka Tucta Tanzania Bi Nasra Khalid Shargy, amekutana na Makundi mbali mbalimbali pamoja na vyama vya wafanyakazi.
Katika kikao hicho cha siku mbili kilichofanyika mkoani Dodoma na kwa siku mbili kuanzia Novemba 13 hadi 14 mwaka huu katika Hoteli ya Dodoma City Hotel na kushirikisha Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu.
Aidha vyma vingine vilivyoshirikishwa ni Chama cha wa Fanya kazi,wahifadhi,hoteli, majumbani,huduma Za jamii na ushauri( CHODAWU), Chama cha wa Ajira Tanzania (ATE), pamoja na ILO kwa lengo la kuendeleza majadiliano yenye tija ili kutathmini maendeleo yaliyofikiwa hadi sasa katika kuelekea utekelezaji wa Mkataba wa ILO wa Wafanyakazi wa Ndani wa mwaka 2011 (No189).