Breaking

Thursday, 16 November 2023

NAIBU WAZIRI MKUU DOTO BITEKO AIPONGEZA TAASISI MAMA ONGEA NA MWANAO KUWAFIKIA WANAFUNZI VIJIJINI

Na Mwandishi Wetu

NAIBU Waziri Mkuu Doto Biteko ameipongeza Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao kwa kazi kubwa wanayofanya katika maeneo ya vijijini ambapo imekuwa na kampeni ya kuwezesha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kupatiwa misaada ya vifaa vya shule hasa viatu.

Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao inayoongozwa na msaniii nguli wa filamu nchini Steven Mengele maarufu Steve Nyerere imekuwa ikitoa vifaa vya shule kupitia Kampeni ya Samia Nivishe Viatu.

Akizungumza leo Novemba 16, 2023 Naibu Waziri Mkuu Biteko ambaye pia ni Waziri wa Nishati amesema Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao imefanikiwa kufika maeneo mengi vijijini na kugusa maisha ya wananchi wenye uhitaji wakiwemo wanafunzi.

Aidha ametumia nafasi hiyo mbali ya kuipongeza taasisi hiyo ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan kwa upendo wake wa kuhakikisha wanafunzi wa Tanzania wanavaa viatu, elimu bure mazingira bora.

"Tunamshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa upendo wake mkubwa wa kuhakikisha wanafunzi wa Tanzania wanapata elimu bila malipo , wanavaa viatu pamoja na kuwekewa mazingira mazuri ya kielimu.Lakini niwapongeze Taasisi ya Mama Ongea na mwanao kwa namna mnavyowafikia wananchi wetu huko vijijini."

Kwa kukumbusha taasisi ya Mama Ongea na mwanao imekuwa ikiendesha kampeni maalumu ya Samia nivishe kiatu yenye lengo la kuwawezesha wanafunzi kupata viatu lakini wakati huo kuwawezesha sare za shule lengo kuhakikisha wanaungana na Serikali inayoongozwa na Rais Samia kutumiza ndoto za watoto wa Tanzania kupata elimu bora katika mazingira rafiki.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages