Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Omolo, akifungua mafunzo ya Kamati za Ukaguzi za mafungu yote yaliyopo Makao Makuu ya Wizara ya fedha kuhusu Mwongozo wa Udhibiti wa Ndani wa Wizara hiyo, yanayofanyika Mkoani Morogoro, ambapo amesisitiza usimamizi madhubuti wa fedha za umma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi ya Fungu Moja (Vote 001) linalohusika na usimamizi wa Deni la Taifa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango TAMISEMI, Bw. John Cheyo, akimshukuru Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Omolo (katikati), kwa kuandaa Mwongozo wa Udhibiti wa Ndani wa Wizara katika kuboresha ukaguzi wa ndani, wakati wa kufungua mafunzo kuhusu mwongozo huo yaliyofanyika Mkoani Morogoro. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani wa Wizara hiyo, Bw. Evarsto Mwalongo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi ya Fungu Moja (Vote 001) linalohusika na usimamizi wa Deni la Taifa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango TAMISEMI, Bw. John Cheyo, akimwongoza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Omolo, alipowasili kufungua Mafunzo ya Kamati za Ukaguzi za mafungu yote yaliyopo Makao Makuu ya Wizara ya Fedha kuhusu Mwongozo wa Udhibiti wa Ndani wa Wizara hiyo, yanayofanyika Mkoani Morogoro.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Omolo (kushoto) na Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi ya Fungu Moja (Vote 001) linalohusika na usimamizi wa Deni la Taifa, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango TAMISEMI, Bw. John Cheyo, wakisikiliza kwa makini maelezo ya wajumbe wa Mafunzo ya Kamati za Ukaguzi za Mafungu yote yaliyopo Makao Makuu ya Wizara ya Fedha (hawapo pichani) kuhusu Mwongozo wa Udhibiti wa Ndani wa Wizara hiyo, yanayofanyika Mkoani Morogoro.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Omolo (wa pili kulia, waliokaa) na Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi ya fungu Moja (Vote 001) linalohusika na usimamizi wa Deni la Taifa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango TAMISEMI, Bw. John Cheyo (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti ya maandalizi ya Mafunzo ya Kamati za Ukaguzi za mafungu yote yaliyopo Makao Makuu ya Wizara ya Fedha kuhusu Mwongozo wa Udhibiti wa Ndani wa Wizara hiyo, yanayofanyika Mkoani Morogoro.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Omolo (wa pili kulia, waliokaa) na Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi ya Fungu Moja (Vote 001) linalohusika na usimamizi wa Deni la Taifa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango TAMISEMI, Bw. John Cheyo (kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mafunzo hayo na wawezeshaji kutoka Kampuni ya KPMG walioshiriki kuandaa Mwongozo wa Udhibiti wa Ndani wa Wizara hiyo, Mkoani Morogoro.
Mjumbe kutoka Kampuni ya KPMG, Bi. Peninah Musya, akitoa mada wakati wa Mafunzo ya Kamati za Ukaguzi za mafungu yote yaliyopo Makao Makuu ya Wizara ya Fedha kuhusu Mwongozo wa Udhibiti wa Ndani wa Wizara ya Fedha, Mkoani Morogoro.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Morogoro)