Breaking

Wednesday, 1 November 2023

MRADI WA MAJI BANGULO WASAINIWA RASMI

Utiaji saini wa kuanza kwa Mradi wa ujenzi wa miundombinu ya usambazaji Maji Dar es salaam ya Kusini umesainiwa leo kati ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) na Mkandarasi Kampuni ya Sinohydro Corporation Ltd na kushuhudiwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Ndugu Kiula Kingu.

Mradi huu utahusisha ujenzi wa tanki kubwa la kuhifadhi maji la lita milioni 9, ujenzi wa kituo cha kusukuma maji na ulazaji wa bomba kwa umbali wa kilomita 25 na unategemea kunufaisha wananchi takribani 450,000 katika majimbo ya uchaguzi ya Kibamba, Segerea, Ukonga, Ubungo,Temeke na Ilala.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages